HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, May 11, 2018

MWENYEKITI WA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM RAIS DKT. MAGUFULI AKIWA KATIKA OFISI NDOGO ZA CCM LUMUMBA JIJINI DAR ES SALAAM


 Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda wakiwaaga Maofisa na Askari Polisi huku wakisukumwa katika gari maalumu wakati wa Gwaride lililoandaliwa kwa ajili ya kuwaaga rasmi baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi.Gwaride hilo lilifanyika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akizungumza na IGP Mstaafu Omar Mahita wakati hafla maalum ya kuwaaga  Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam. (Picha na Jeshi la Polisi).
 Kamishna Mstaafu wa Polisi Clodwing Mtweve akikagua gwaride lililoandaliwa kwa heshima yake wakati wa hafla maalum ya kumuaga baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam  (Picha na Jeshi la Polisi).
 Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla maalum ya kuwaaga rasmi Jeshini baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).
 Askari wa Kikosi cha Kutuliza ghasia FFU wakitoa heshima wakati  wa gwaride maalam la kuwaaga Makamishna wastaafu wa Jeshi la Polisi, Clodwing Mtweve na Elice Mapunda baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro akifurahia jambo na Makamishna wastaafu Clodwing Mtweve (katikati) na Elice Mapunda (kushoto) wakati wa hafla maalum ya kuwaaga baada ya kustaafu utumishi ndani ya Jeshi la Polisi. Hafla hiyo ilifanyika katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es Salaam (Picha na Jeshi la Polisi).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad