Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
SHIRIKA la kuhudumia Viwanda Vidogo vidogo(SIDO),limetoa vyeti vya kutambua viwanda vidogo vidogo na vya kati kwa wamiliki na wajasiriamali zaidi ya 300 kwa Mkoa wa Dar es Salaam.
Tukio la utoaji vyeti hivyo umefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo aliekabidhi vyeti vya kuwatambua wamiliki na wajasiriamali wa viwanda hivyo ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ambaye alipaswa kuwa mgeni rasmi.
Kabla ya kutolewa kwa vyeti hivyo vya kuvitambua viwanda hivyo vidogo na vya kati kwa Mkoa wa Dar es Salaam imelezwa kuna wajasiriamali 600 na kati yao ndio hao wamepewa vyeti ili kutambua viwanda vyao na mchango wao katika jitihada za kuleta maendeleo kuelekea Serikali ya viwanda nchini.
Akizungumza kwenye tukio hilo lililohudhuria na mamia ya wajasiriamali wa mkoa huo, Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Lyaniva amesema SIDO wamefanya tukio la kihistoria kwa kutambua mchango wa wamiliki wa viwanda hivyo na kuongeza Serikali kwa upande wake itazifanyia kazi changamoto za wajasiriamali hao.
"Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye ndiye mgeni rasmi kwenye tukio hili na mimi nimemwakilisha kutokana na majukumu aliyonayo, amenituma nifikishe salamu zake kwenu.Kwanza anatoa pongezi na shukrani kwa Mkurugenzi Mkuu wa SIDO kwa kuendelea na majukumu yao ya kuwasimamia wajasiriamali wadogo na wakati ili watimize malengo yao.
"Sote tunafahamu Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi mahiri wa Rais Dk.John Magufuli pamoja na mambo mengine umejikita kuhakikisha tunafanikiwa katika viwanda na ili kufanikisha malengo hayo mchango wa SIDO unahitajika sana.
"Leo jumla ya viwanda 300 kati ya 600 vilivyopo Mkoa wa Dar es Salaam wamiliki wake wanakabidhiwa vyeti vya kutambuliwa na SIDO.Hii ni hatua nzuri kwa maendeleo ya nchi yetu na changamoto ambazo zimeanishwa na wajasiriamali niahidi zitafanyiwa kazi kwa Serikali yetu ni sikivu,"amesema.
Moja ya ya changamoto ni wajasiriamali kukosa maeneo ya kufanyia shughuli zao, hivyo ameahidi kufikisha ombi lao kwa Mkuu wa Mkoa na kueleza kuna meneo makubwa Kigamboni wanayoweza kutolewa kwa wajasiriamali hao wayatumie shughuli zao za uzalishaji bidhaa.
Wakati huohuo amewaomba wamiliki hao wa viwanda kutokuwa na masharti magumu katika kutoa ajira na kufafanua wilayani kwake anayo kesi ya muajiri kudaiwa kung'ang'ania vyeti halisi vya kitaaluma vya mtu aliyemuajiri.
"Niwaombe msiwe na mashrti magumu kwa mfano hili la kuchkua vyeti vya mtu ni sharti ambalo sijawahi kuliona mahali popote pale duniani,"amesisitiza.
Pia amewataka wamiliki hao wa viwanda kuhakikisha wanatenda haki kwa wanaowaajiri ili kuondoa migogoro kati ya muajiri na muajiriwa ambayo inarudisha nyuma jitihada mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lyaniva (mwenye sharti la mikono mirefu),akikata utepe katika mfao wa cheti ikiwa ni kuashiria kuanza kwa tukio la utoaji vyeti vya kutambua viwanda vidog vidogo 300 jijini.Vyeti hivyo vimetolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo vidogo(SIDO).
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akisoma maelezo yaliyokuwa kwenye mfano wa cheti ambacho kimeandaliwa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo(SIDO) kwa ajili ya kuwakabidhi wamiliki na wajasiriamali ambao wanamiliki viwanda vidogo na vya kati jijini Dar es Salaa.Tukio hilo limefanyika leo.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva akikabidhi cheti kilichotolewa na Shirika la Viwanda Vidogo vidogo(SIDO) kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa PSPF Adam Mayingu(wa kwanza kushoto) kwa niaba ya Mfuko huo leo jijini Dar es Salaam. Pia SIDO imetoa vyeti hivyo kwa wamiliki na wajasiriamali wa viwanda wapatao 300 kati ya wajasiriamali 600 wa mkoa huo wanataotambuliwa na shirika hilo.
Baadhi ya wamiliki na wajasiriamali wa viwanda vidog na vya kati wakiwa wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam Felix Lyaniva kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda wakati wa utoaji vyeti vya kutambua viwandao vidogo na vya kati 300 katika mkoa huo ambavyo vimetolewa na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo(SIDO) leo jijini.
No comments:
Post a Comment