HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, April 11, 2018

BONGO MOVIE KUIBUA VIPAJI VIPYA NA KUHUBIRI AMANI, UPENDO NA UZALENDO TANZANIA


Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza ambaye ni Mratibu wa Tamasha la Iringa ya Kwetu, Kijana Amka tufanye kazi, Steve Nyerere akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuelezea Tamasha la 'Iringa ya Kwetu, Kijana Amka tufanye kazi,' Pembeni (kushoto) ni Msanii Shamsa Ford na kulia ni Msanii Wolper.
Wasanii waliohudhuria utambulisho wa Tamasha la 'Iringa ya Kwetu, Kijana Amka tufanye kazi.
Msanii wa maigizo na filamu nchini, Single Mtambalike maarufu kwa jina la Richie akifafanua machache. Na Mwandishi Wetu. Kundi la Wasanii wa Muziki, Bongo Fleva, Mziki wa Singeli na Filamu nchini wanataraji kutoa elimu ya kujikwamua kiuchumi vijana wa Iringa katika Viwanja vya Mwembe Togwa mkoani Iringa.

Akizungumza wakati wa utambulisho wa Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza ambaye ni Mratibu wa Tamasha la Iringa ya Kwetu, Kijana Amka tufanye kazi, Steve Nyerere amesema kuwa Tamasha hilo lenye kauli mbiu ya 'Kijana wa Iringa inuka tukafanye kazi,'.

“Tunataka tuwaonyeshe vijana kuwa huyu Wolper, JB au Steve Nyerere awakuwa wasanii maarufu moja kwa moja bali kuna maisha walipitia mpaka kufikia hapo hivyo wanatakiwa kufanya kazi ili waweze kufikia mafanikio kutoka kijiweni na kuwa wajasilimali kama walivyo hawa wasanii wakubwa” amesema Steve.

Kwa upande wake Msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu nchini, Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven 'JB amesema wanafika Iringa kwa lengo moja tu la kuhakikisha wanaonana na wasanii na vikundi vya Iringa kwa lengo la kutaka kuwainua kitaaluma kwa kuwapa uzoefu ambao wameupata kwa zaidi ya miaka 20.

Amesema tunajua kuna wasanii wengi sana huku mikoani lakini je ni muda gani wanapata nafasi hivyo wanakwenda Iringa na wataacha mabalozi ambao ndio watakuwa maharufu katika kizazi kijacho cha filamu.

Kwa upande wake Msanii maharufu wa kike wa filamu nchini, Jackline Wolper amesema umaharufu hauzuii kufanya mambo ya msingi kama ujasiliamali ili aweze kujiongezea kipato.

Amesema kuwa licha ya kuwa maarufu bado amekuwa akijihusisha na ufundi cherehani kama sehemu ya kujiongezea kipato katikamaisha yake ya kila siku.
Msanii Jackline Wolper akifafanua machache.
Mwenyekiti Steve akitoa ya Moyoni.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad