HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 5, 2018

CHIRWA, KAMOSOKU KAMILI GADO KUWAVAA WABOTSWANA KESHO

Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa akizungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Townshio Rollers utakaopigwa kwenye dimba la Uwanja wa Taifa.

Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.

Uongozi wa klabu ya Yanga umesema kwamba kikosi chao kimejiandaa vyema kuwakabili Township Rollers ya Botswana hapo kesho katika mchezo wao wa klabu bingwa barani Afrika utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kuanzia mishale ya saa 10 na nusu jioni.

Katibu mkuu wa klabu ya Yanga,Charles Boniphace Mkwasa amesema kwamba hali ya wachezaji iko vizuri kwa ajili ya pambano hilo na jambo la faraja ni kurejea kwa baadhi ya wachezaji wao ambao awali walikuwa majeruhi akiwemo Obrey Chirwa na Thabani Kamusoko.

Mkwasa alisema kwamba kuelekea katika mchezo huo itategemea na mipango ya mwalimu kama ataweza kuwajumuisha wachezaji hao ambao walikuwa majeruhi katika pambano hilo linalotaraji kuwa na ushindani wa hali ya juu.

Aidha alisema kwamba licha ya kurejea kwa wachezaji Donald Ngoma, Amisi Tambwe na Vicent Andrew katika kikosi ila bado hawapo katika mipango ya mwalimu kwa ajili ya mechi ya kesho hivyo huenda wakatumika katika mechi ya marudiano itakayochezwa nchini Botswana.

Hata hivyo Mkwasa alisema kwamba wataingia katika mchezo huo kwa tahadhari kubwa kwa kuwa wanakutana na timu ngumu iliyo bora kwenye mashindano hayo makubwa kwa ngazi ya vilabu barani Afrika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad