HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, March 7, 2018

BARAZA LA MADIWANI KINONDONI LAPITISHA BAJETI YA MWAKA 2018/2019

Na Emmanuel Masaka, Globu ya Jamii
BARAZA  la Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam kupitia mkutano wake maalum limepitisha makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida  na mpango wa maendeleo kwa mwaka 2018/2019.

Ambapo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatarajiwa kukusanya na kupokea Sh. 242,185,292,987.00 ambapo Sh. 209,436,308,079.00 sawa na asilimia 86.5 ni ruzuku kutoka Serikali kuu.

Wakati Sh. 686,380,000.00  sawa na asilimia 0.3 ni mchango wa jamii na  Sh. 32,062,704,908.00 sawa na asilimia  13.2 ni mapato ya ndani ya manispaa.

Akizungumza mbele ya Madiwani wa Manispaa hiyo katika kikao hicho jana, Meya wa Manispaa ya Kinondoni Benjamini Sitta amesema kati ya fedha hizo zilizopitishwa, Sh. 120,326,705,873.00 ni matumizi ya kawaida ambayo ni sawa na asilimia 49.7 ya bajeti yote.

Amesema Sh. 121,858,587,114.00 ni fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo ambayo ni sawa na asilimia 50.3 ya bajeti.

 Meya Sitta ameeleza kuwa atika fedha hizo Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni inatarajia kukusanya Sh. 32,749,084,908.00 kutoka vyanzo vyake vya ndani.

"Sh. 16,392,166,400.00 zitatumika kwa matumizi ya kawaida na Sh. 16,356,913,508.00 zitatumika kwa ajili ya miradi ya maendeleo na  fedha za ruzuku kutoka Serikali kuu ni Sh. 209,436,208,079.00 zitakazojumuisha Sh. 105,501,668,606.00 kwa  ajili ya miradi ya maendeleo," amesema.

Sitta amefafanua mishahara ya watumishi kutokana na mapato ya ndani ni Sh. 906,498,855.00 na mishahara kutokana na ruzuku ya Serikali Kuu ni Sh. 99,590,270,811.00.

Hivyo inafanya jumla ya Sh. 100,496,769,666.00 fedha kwa matumizi mengineyo ni Sh. 15,485,667,545.00 kutoka vyanzo vya ndani na Sh.4,344,268,662.00 kutoka ruzuku ya Serikali kuu na kufanya jumla ya matumizi mengineyo kuwa ni shilingi 19,829,936,207.00.

"Ili kufikia mafanikio yaliyokusudiwa Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni itaimarisha mahusiano mazuri kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wadau wengine itaendelea kujenga uwezo na ujuzi kwa watumishi katika utoaji wa huduma  zilizo bora.

" Madiwani na  wenyeviti wa Serikali ya Mitaa nao  watakuwa mstari wa mbele katika kusimamia  shughuli za wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,"amesema.

Aidha mpango wa matumizi nabajeti ya mwaka 2018/2019 ni sehemu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) ya mwaka 2015-2020.

Hivyo matokeo ya utekelezaji wa  mpango na bajeti yameelekezwa katika kujibu matarajio ya watu ambayo ni utatuzi wa  kero zao pamoja na maisha bora kwa kila mtanzania,"amesema Sitta.
  Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Mhe. Benjamini Sitta akizungumza mbele ya Madiwani wa Manispaa hiyo  katika mkutano maalumu wa Baraza leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Madiwani wakimsiliza Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe. Benjamini Sitta. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad