Naibu
 Waziri wa Maji na Umwagiliaji Jumaa Aweso amesema Serikali ya Rais 
Magufuli kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji imetoa kipaumbele kwa 
viwanda vya ndani vinavyozalisha bidhaa zinazotumika kutekeleza miradi 
mikubwa ya maji inayoendelea kujengwa nchini kote.
Aweso
 ametoa kauli hiyo mjini Kahama alipotembelea kiwanda cha Kahama Oil 
Mills, mkoani Shinyanga ambacho moja ya shughuli zake ni kutengeneza 
mabomba na vifaa mbalimbali vinavyotumika kutekeleza miradi ya maji na 
kutoa angalizo kwamba ni lazima viwanda vya ndani vizingatie ubora wa 
bidhaa zao na kukidhi mahitaji halisi ya miradi yote ya maji nchini.
‘‘Hatuna
 sababu ya kutotumia bidhaa zinazozalishwa na viwanda vyetu vya ndani, 
maadamu vinazingatia ubora wa bidhaa inazozalisha na kukidhi mahitaji ya
 nchi yetu. Serikali ya Rais Magufuli imetoa kipaumbele kwa wazalendo 
nchini, hivyo tumieni fursa hii na kutomuangusha,’’ alisema Aweso.
Meneja
 wa Kahama Oil Mills, John Zimudo kwa upande wake akizungumza wakati wa 
ziara hiyo anasema amefarijika sana kwa ujio wa Naibu Waziri wa Maji na 
Umwagilaji, na kutoa shukurani kwa Serikali ya Awamu ya Tano za kuunga 
mkono juhudi za wazawa katika kuinua Sekta za Viwanda nchini, huku 
akiahidi kutekeleza azma ya Rais Magufuli ya kujenga Tanzania ya Viwanda
 kwa vitendo.
Aidha,
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso amekagua hatua ya 
utekelezaji wa mradi wa maji wa pamoja (Joint Water Partnership Project)
 unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu na
 halmashauri za wilaya ya Shinyanga na Msalala kwa mkoa wa Shinyanga na 
Nyangh'wale kwa Mkoa wa Geita.
Mradi
 huo ukikamilika utahudumia vijiji 13 vya Mwenge, Nyugwa, Kharumwa, 
Mwamakiliga, Izunya, Kafita, Lushimba, Rwabakanga, Kakola namba 9, 
Bushingwe, Kakola, Bugarama, na Ilogi.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akipokea maelekezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Kiwanda cha Kahama Oil Mills, Jiten Divecha (kulia) ambacho moja ya shughuli zake ni kuzalisha vifaa vya maji kilichopo wilayani Kahama, mkoani Shinyanga alipotembelea kiwandani hapo.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akihakiki ubora wa maji yanayozalishwa na mradi wa pamoja (Joint Water Partnership Project) unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu na halmashauri za wilaya ya Shinyanga na Msalala kwa mkoa wa Shinyanga na Nyangh'wale kwa Mkoa wa Geita.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Kakola ambacho ni miongoni mwa vijiji 13 vitakavyonufaika na mradi wa pamoja (Joint Water Partnership Project) unaotekelezwa kwa ushirikiano kati ya mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu na halmashauri za wilaya ya Shinyanga na Msalala kwa mkoa wa Shinyanga na Nyangh'wale kwa Mkoa wa Geita.
 Baadhi ya mabomba yanayozalishwa na Kiwanda cha Kahama Oil Mills kilichopo wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.





No comments:
Post a Comment