Na Mwandishi wa Globu ya Jamii, Same.
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule amekutana na Maofisa wa jeshi la Polisi na watendaji wa jeshi hilo kuzungumzia namna ya kuimarisha Ulinzi Na usalama wa Raia katika Mwaka 2018 sambamba na kufanya tathmini ya utendaji kazi kwa mwaka 2017.
Katika Mkutano huo DC Sinyamule alipata nafasi ya kusikiliza changamoto za jeshi la Polisi wa Wilaya hiyo na kuahidi kuzifanyia kazi katika kipindi kifupi ili waweze kuongeza ufanisi kwenye kazi zao za kila siku.
Aidha alitumia Mkutano huo kama sehemu ya kuwapongeza na kuwashukuru kwa kazi Nzuri waliyoifanya mwaka 2017 iliyopelekea kupungua kwa matukio ya uhalifu, kudhibiti ajali za barabarani na kupambana na dawa za kulevya kama mirungi ambayo hapo awali ilikuwa ikipitishwa kwa wingi kupitia njia za panya katika Wilaya hiyo.
Dc Sinyamule Aliwakumbusha jeshi la Polisi kuhakikisha wananchi wanakaa kwa amani na utulivu. Kama wajibu wa kwanza kwa serikali na kuwataka kuacha kujihusisha na tamaa za upokeaji wa rushwa wa aina yoyote ile kwani kwa kufanya hivyo kutapunguza weledi wa kazi yao.
Pia alimaliza kwa kutoa ahadi ya kuanzisha tuzo kwa kutoa lakini 5 kila miezi 3, ili askari wanaofanya vizuri wapewe na kuwanunulia tanki la Maji kwa ajili ya kituo hicho cha Polisi cha Wilaya ya Same .
" Mh. Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli anapohimiza maendeleo na watu kufanya kazi, lazima sisi tuhakikishe uwepo wa amani na utulivu ili kazi hizo ziweze kufanyika" Amesema DC Sinyamule.
Mkuu wa Wilaya ya Same, Rosemary Sinyamule(katikati) akiandika jambo katika kikao chake na jeshi la Polisi la Wilaya hiyo juu ya kudhibiti hali ya ulinzi na Usalama .
Baadhi ya Maofisa na Watendaji wa jeshi la Polisi waliohudhuria Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Same na Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na Usalama
Baadhi ya Maofisa na Watendaji wa jeshi la Polisi waliohudhuria Mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Same na Jeshi la Polisi katika kuimarisha ulinzi na Usalama
No comments:
Post a Comment