Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina akisoma stakabadhi ya malipo ya sh 50,000 kwa kila ng’ombe kinyume cha sheria aliyotozwa mfugaji wa Kijiji cha Handa, Tulway Bombo ambapo Waziri Mpina alitangaza kufuta maamuzi hayo na kuamuru wafugaji hao kurudishiwa fedha zao.
Na John Mapepele
Na John Mapepele
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amefuta tozo ya faini ya shilingi elfu
hamsini kwa kila Ng’ombe mmoja na ameuagiza Uongozi wa Wilaya ya Singida
kuwarudishia mara moja fedha wafugaji wote walizotozwa faini kinyume cha
Sheria katika zoezi la kukamata mifugo linaloendelea katika Hifadhi ya Msitu wa
Jamii wa Mgori.
Waziri Mpina ametoa maelekezo hayo leo alipotembelea eneo la Hifadhi ya Msitu
wa Jamii wa Mgori, kwenye Kijiji cha Handa na kuwaagiza Wakuu wa Mikoa ya
Singida na Dodoma kupitia kwa Wakuu wa Wilaya ya Singida na Chemba
kushirikiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo anayeshughulikia Sekta ya
Mifugo, Dkt. Mary Mashingo kufika katika eneo hilo kabla ya tarehe15/12/2017
kushughulikia mipaka baina eneo la Singida na Handa kwa upande wa Wilaya ya
Chemba na migogoro ya wafugaji inayoendelea.
“Kama Waziri mwenye dhamana ya kushughulikia Sekta ya Mifugo na Uvuvi nchini
sipo tayari kuvunja Sheria kwa kuwakumbatia wahalifu wanaokiuka Sheria za nchi
kwenye Sekta ya Mifugo na Uvuvi, lakini pia wahalifu wanatakiwa kutozwa faini
kulingana na Sheria na taratibu zilizowekwa. Utozaji wa faini ambao hauzingatii
hili ni uvunjaji wa Sheria “ alisisitiza Mpina.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Handa Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma baada ya kufika kijijini hapo kisha kuamuru wafugaji waliokamatiwa mifugo yao na kutozwa faini ya sh 50,000 kila ng’ombe warudishiwe kiasi cha sh. 30,000 kutokana na faini hiyo kutozwa kinyume cha sheria.
Waziri Mpina alisema utozaji wa faini wa shilingi 50,000/= toka shilingi 20,000/=
za awali kwa kila Ng’ombe aliyekamatwa na shilingi 25,000/= kwa Mbuzi toka
shilingi 5,000/= za awali haukubaliki na kumuagiza Mkuu wa Wilaya ya Singida,
Elias Tarimo kurudisha shilingi 30,000/= kwa kila Ng’ombe ambazo zimetozwa
bila kufuata Sheria yoyote.
Baadhi ya wafugaji waliofika katika kijiji cha Handa kulalamikia tozo ya shilingi
50,000 kwa kila Ng’ombe mmoja walizotozwa na Halimashauri ya Wilaya ya
Singida ni pamoja na Jerumani Waline aliyetozwa jumla ya shilingi 2,500,000/=,
kwa idadi ya mifugo 66, Mabula Mwala aliyetozwa shilingi 1,950,000/= kwa idadi
ya mifugo 45, Joel Tahan aliyetozwa jumla ya shilingi 1,000,000/= kwa idadi ya
mifugo 31, Elizabeth Hamisi aliyetozwa shilingi 1,050,000/= kwa idadi ya mifugo
34,na Elizabethi Nyambi aliyetozwa jumla ya shilingi 350,000/= kwa idadi ya
mifugo 8.
Akizungumza kwa niaba ya wafugaji bwana Jerumani Waline, amesema
changamoto kubwa kwa sasa ni kuainishwa kwa mipaka ya Kijiji cha Handa na
Hifadhi ya Msitu wa jamii wa Mgori na eneo la kunyeshea maji mifugo ambapo
alimuomba Waziri kulishughulikia suala hilo.
Waziri Mpina ameiagiza Halmashauri ya Singida kupitia mara moja tozo hizo na
kuzipeleka kwenye Mamlaka husika ili zipitishwe na kuanza kutumika kwa taratibu
zinazokubalika kisheria.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Luhaga Mpina akimsikiliza kwa makini Mkazi wa Kijiji cha Handa wilayani Chemba, Jumanne Sadick kuhusu tatizo la mpaka kati ya Pori la Hifadhi ya Swagaswaga na Mgori ambapo Waziri Mpina aliagiza ifikapo Disemba 15 mwaka huu Katibu Mkuu Mifugo na viongozi wa Mkoa wa Singida na Dodoma kufika eneo hilo ili kuupatia ufumbuzi mgogoro huo.
Pia amezitaka Halimashauri zote nchini kutojiingiza katika mtego wa kutoza faini
ambazo hazipo kisheria kwa kuwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria na kuagiza
kuwa kuanzia sasa Halimashauri zote zinatakiwa kutoa taarifa kwa Wizara ya
Mifugo na Uvuvi pindi zinapotaka kuendesha operesheni za mifugo ili kuwa na
ufahamu wa pamoja baina ya Wizara na wadau wengine hali ambayo itasaidia
kuboresha operesheni hizo na kuondoa migongano isiyo ya lazima.
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI
No comments:
Post a Comment