Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
Naibu
Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega amesema kuwa changamoto ya
wataalam katika halmashauri ya Mkuranga itamalizwa pale wanamkuranga
wakiamua kusomesha watoto ambao ndio watakuwa watumishi wa halmashauri
hiyo.
Ulega ameyasema hayo wakati
akizindua madarasa ya awali katika shule ya Msingi Magoza, amesema uwepo
wa changamoto ya walimu na wataalam wengine ni kutokana wanamkuranga
kushindwa kutoa kipaumbele katika kusomesha watoto.
Amesema kuwa shule ya awali hiyo ni kwa ajili ya kumuandaa mtoto ili aweze kupata muongozo pale anapoanza darasa la kwanza .
Ulega
amesema wananchi wa Mkuranga kwa sasa wanahitaji kuamka katika
kusomesha watoto kutokana hali ya uchumi wa viwanda inahitaji wa kada
mbalimbali ndio watakaotumikia uchumi huo bila kufanya hivyo basi
wakaotumika katika viwanda hivyo ni kutoka sehemu nyingine kutokana na
kuwa na sifa ya kufanya katika viwanda.
Amesema
shule zipo cha kufanya wananchi ni kuhimiza kusoma watoto na serikali
imeweka mkazo ikiwa ni pamoja na kutoa elimu bure ili kila mtu aweze
kusoma bila kuwepo kwa kisingizio cha uwezo wa kifedha.
Aidha amesema kutokana ufadhili wa shule ya awali magoza na sehemu nyingine ambayo mfadhili atapita asiwekewe vikwanzo.
Nae
Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Mkuranga, Ally Msikamo amesema kuwa kazi
ya chama ni kusimamia ilani iweze kutekelezeka kama walivyoahidi katika
kampeni 2015.
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Magoza katika hafla ya uzinduzi wa madarasa ya awali katika shule ya msingi Magoza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid akizungumza mipango ya halmashauri juu ya uboreshaji wa elimu katika Wilaya ya Mkuranga.
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega akizindua vyumba vya madarasa ya awali katika shule ya Msingi Magoza.
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Magoza wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega.
Mwonekano wa Madarasa ya awali katika shule ya Msingi Magoza.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid akizungumza mipango ya halmashauri juu ya uboreshaji wa elimu katika Wilaya ya Mkuranga.
Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega akizindua vyumba vya madarasa ya awali katika shule ya Msingi Magoza.
Sehemu ya wananchi wa Kijiji cha Magoza wakimsikiliza Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo, Abdallah Ulega.
No comments:
Post a Comment