Na Mwandishi Wetu.
Wananchi
wa Wilaya ya Gairo wameombwa kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika
maendeleo ya sekta ya elimu ili kupata matokeo bora.
Kauli
hiyo imetolea Disemba 21, 2017 wakati wa kuwasomea mapato na matumizi
ya michango ya elimu kwa wananchi wa Kata ya Chakwale na Mkuu wa Wilaya
ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe wakati akabidhi tani mbili na nusu
ya mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno.
Mhe.
Mchembe alisema kuwa saruji hiyo itasaidia kuendeleza zoezi la kufyatua
matofali ambapo mpaka sasa wameshafyatua matofali 5,600.
Aidha amekaribisha wadau mbalimbali kuendelea kuchangia baada ya wananchi kuchangia shilingi milioni 33 ndani ya miezi mitatu.
"Hamasa
ni kubwa kwani watoto wanatembea kilometa zaidi ya Sita kwenda shule.
Hili limekuwa ni jaribu kwa watoto wa kike. Vijana wa bodaboda
wanatuharibia watoto wa kike. Shule ikiwa karibu itapunguza changamoto
hii.
Mkuu
wa Wilaya aliipongeza Kamati ya Ujenzi kwa kazi nzuri ya kukusanya
michango ya maendeleo na kazi ya ujenzi ambayo tayari imeanza.
Tunategemea kuanza ujenzi mapema Januari katika eneo la ekari 15.
Wilaya
ya Gairo ina madarasa zaidi ya 30 yote yamejengwa kwa nguvu ya wananchi
hadi ngazi ya boma, bado kuezeka. Madarasa haya ni nje ya madarasa 16
yaliyomalizika ndani ya mwaka mmoja.
"Mpaka
sasa hatuna darasa la nyasi wala wanafunzi wanaokaa chini. Tumemaliza
nyumba za waalimu 8, maabara 6 na tuna maboma yanahitaji nguvu ya
ziada," alisema.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akimkabidhi mifuko ya saruji kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili iweze kusaidia katika ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu na nyumba za walimu. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo.
Wananchi wa Kata ya Chakwale wakisomewa taarifa ya michango yao shilingi milioni 33. Aidha Wenyeviti wa vijiji vitatu walirudishiwa shilingi milioni 10 ikiwa ni kwa ajili ya shughuli za Maendeleo ya vijijini.
Mkuu wa Wilaya akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Mhe. Maneno ili awagawie Wenyeviti.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mhe. Siriel Shaidi Mchembe akikabidhi hundi ya milioni kumi kwa Diwani wa Chakwale Mhe. Maneno ili ili awagawie Wenyeviti wa kata yake. Mkutano huo ulifanyika Disemba 21, 2017 katika Kata ya Chakwale, Gairo.
No comments:
Post a Comment