
Kiongozi msaidizi wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu (HDIF), Joseph Manirakiza akimkabidhi barua ya makabidhiano ya mradi na vifaa mganga mkuu wa hospital ya Shirati, Dr. Bwire Chiragi kwa muda wa miaka miwili hospitali hiyo imepata ufadhili wa kuendesha mradi wa kuokoa maisha ya mama na mtoto (saving mothers project) katika wilaya za Bunda na Tarime mkoani Mara.
Mganga mkuu wa hospitali ya Shirati, Dr. Bwire Chiragi akisaini makabidhiano ya mradi wa kuokoa maisha ya mama na mtoto (saving mothers project) katika wilaya za Bunda na Tarime mkoani Mara. Katikati ni kiongozi msaidizi wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu (HDIF), Bw Joseph Manirakiza na Kulia ni Katibu wa hospitali ya Shirati, Ogottu Obala.
Msaidizi kiongozi wa Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu (HDIF) , Joseph Manirakiza (katikati) akifafanuliwa jambo na viongozi wa hospitali ya Shirati iliyopo mkoani Mara, kulia ni Mganga mkuu wa Hospitali hiyo, Dr. Bwire Chiragi na kushoto Katibu wa hospitali hiyo, Juma Ogottu Obala
Baadhi ya Baiskeli 124 zilizotolewa na Mfuko wa Ubunifu na Maendeleo ya Watu (HDIF) uliochini ya UKAIDS kwa ajili ya kuwasaidia wauguzi katika Wilaya ya Bunda na Tarime.
Mama Prisca Koboko Ambae ni muuguzi toka Tarime akielezea jinsi mradi wa kuokoa maisha ya mama na mtoto ulivyowawezesha kuwafikia wakina mama.

Mama Teodocia James, wa kwanza kushoto ni mmoja ya wamama walionufaika na huduma za mradi huu wa 'Saving Mothers' uliopata ufadhili wa HDIF kwa karibu shilingi bilioni moja ya Tanzania akielezea jinsi mradi ulivyookoa maisha yake.

No comments:
Post a Comment