Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akitia saini Nyaraka zenye majina ya Wafungwa 61
waliohukumiwa kunyongwa pamoja na majina mawili ya Familia ya Nguza
Viking (Babu Seya), na Johnson Nguza waliopata msahama wa Rais, katika
Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kulia ni Kamishna Jenerali wa
Magereza Dkt. Juma Malewa akishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiyahakiki kwa kuyasoma majina ya Wafungwa 63
waliopata msahama wa Rais kabla ya kutia saini Nyaraka hizo za Msamaha
katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma. Kulia ni Kamishna Jenerali wa
Magereza Dkt. Juma Malewa akishuhudia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiagana na Kamishna Jenerali wa Magereza nchini Dkt.
Juma Malewa mara baada ya kutia saini majina ya wafungwa 61
waliohukumiwa kunyongwa pamoja na majina mawili ya Wafungwa Nguza
Viking(Babu Seya), na Johnson Nguza waliokuwa wamehukumiwa kifungo
cha maisha jela.
No comments:
Post a Comment