Serikali iko katika hatua za mwisho za kukamilisha mradi wa kufunga Taa za kuongozea ndege
ili kuruhusu Uwanja wa Ndege wa Dodoma kuweza kutumika masaa 24.
Akizungumza hayo mjini Dodoma mara baada ya kukagua Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light) zilizofungwa uwanjani hapo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa uboreshaji wa uwanja huo katika kuruhusu ndege za aina zote kutua masaa 24 kwa wiki.
Akizungumza hayo mjini Dodoma mara baada ya kukagua Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light) zilizofungwa uwanjani hapo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, amesema kuwa hatua hiyo ni muendelezo wa uboreshaji wa uwanja huo katika kuruhusu ndege za aina zote kutua masaa 24 kwa wiki.
Muonekano wa Mfumo wa Kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light),
zilizofungwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Taa hizo zitatumika kuongozea ndege
nyakati za Usiku na zina uwezo wa kuwaka masaa laki moja.
“Hii ni hatua ya pili ya uboreshaji wa uwanja huu ambapo hatua ya kwanza tumeimaliza ya
upanuzi wa barabara za kuruka na kutua ndege (runway) hadi kufikia KM 2.5”, amesema Waziri
Profesa Mbarawa.
Aidha, ameongeza kuwa ufungaji wa taa hizo umegawanywa kwa hatua tatu ambapo awamu ya
kwanza imekamilika kwa kujumuisha ufungaji wa Mfumo wa Kisasa wa Taa za Umeme Jua
(Aviation Solar Powered Light), katika barabara za kuruka na kutua ndege na maeneo ya
maegesho, hatua ya pili ni kufunga taa za kumsaidia Rubani kuweza kuona uwanja wote na
hatua ya mwisho ni taa zitakazofungwa mita 400 kila upande uwanjani hapo.
Amefafanua kuwa Taa hizo za kisasa (Aviation Solar Powered Light) zitapunguza gharama za
uendeshaji uwanjani hapo ikiwemo matengenezo yake kwani zinadumu muda mrefu.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara, Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho,
amesema kuwa nia ya Serikali ni kuendelea kurefusha uwanja huo ambapo italipa fidia kwa
nyumba zilizopo pembeni ya uwanja huo ili kuongeza usalama wa uwanja na ndege kwa
ujumla.
“Tutaweka uzio katika uwanja huu kulingana na matakwa ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege na
pia kupitia uzio huu taa zitakuwa salama”, amesisitiza Dkt. Chamuriho.
Naye, Msimamizi wa mradi Bw. Samwel Mruma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini
(TAA), amesema mfumo wa taa hizo za kisasa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light),
zimefungwa kwa siku 14 na zina uwezo wa kufanya kazi kwa miaka 12 na kuwaka kwa masaa
laki moja ukilinganisha na nyingine ambazo zinawaka kwa masaa elfu kumi.
Mfumo wa uwekaji Taa za Kisasa ni mkakati wa Serikali katika kuhakikisha inaendelea
kuboresha viwanja vyake vya ndege ili kukidhi viwango vianavyostahili katika usafiri wa anga.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), akitoa
maelekezo kwa Msimamizi wa mradi Bw. Samwel Mruma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya
Ndege Nchini (TAA), wakati alipokagua mfumo wa Kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation
Solar Powered Light), zilizofungwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma. Kushoto ni Katibu
Mkuu wa Wizara, Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho na kulia ni Meneja wa Uwanja
huo Julius Mlungwana.
Msimamizi wa mradi Bw. Samwel Mruma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA),
akionesha Taa za Kisasa za Umeme Jua (hazipo pichani), kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (wa pili kulia), zilizofungwa kwa ajili ya kuongozea
ndege katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akionesha kifaa
(Remote Controller) cha kuwashia Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light),
zilizofungwa katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma kwa waandishi wa habari, wakati akikagua
Taa hizo uwanjani hapo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kulia), akitoa
maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara, Sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho (katikati),
na Meneja wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng. Leonard Chimagu (kushoto),
wakati alipokagua mfumo wa kisasa wa Taa za Umeme Jua (Aviation Solar Powered Light),
katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma.
No comments:
Post a Comment