Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos G. Makalla Ahaidi kushughulikia matatitizo ya wafanyakazi yaliyo onekana  uwezo wa mkoa na yale ya kisera atayawasilisha katika wizara au mamlaka husika kwa   wakati.Asema serikali haitomuonea mfanyakazi yeyote katika uwajibishaji au hatua za nidhamu bali serikali itazingatia sheria, kanuni na taratibu za kiutumishi
 Amewataka waajiri kuwasilisha michango ya wafanyakazi katika mifuko ya Hifadhi ya jamii kwa mujibu wa sheria
Aidha amewakumbusha wafanyakazi  haki zao na wajibu wao kwa kufanya kazi kwa bidii
Amewashukuru wafanyakazi na Viongozi wa wafanyakazi kwa kushirikiana na serikali ktk kushughulikia changamoto za wafanyakazi, hayo ni baadhi ya maneno katika hutuba yake kwa wafanyakazi wa mkoa wa mbeya katika sherehe za mei mosi zilizo fanyika kimkoa katika Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.PICHA NA MR.PENGO MBEYA.
Baadhi ya wafanyakazi wa serikali, Taasisi binafsi na waajiliwa wakiwa katika maandamano ya kusherehekea sikukuu ya wafanyakazi Duniani ambayo kimkoa wa mbeya ilifanyika katika uwanja wa sokoine jijini mbeya.


Kocha mchezaji na  Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makalla akionyesha kombe la heshima mara baada ya  kuibamiza bila huruma timu ya viongozi wa Dini kwa mabao 4-1.
Mpira ulikuwa mkali ila timu ya Viongozi wa serikali iilionekana kucheza kwa maelewano hivyo kuisaidia timu hiyo kuibuka mshindi na kumaliza tambo za muda mrefu wa timu hizo.
Mpira ulikuwa mkali ila timu ya Viongozi wa serikali iilionekana kucheza kwa maelewano hivyo kuisaidia timu hiyo kuibuka mshindi na kumaliza tambo za muda mrefu wa timu hizo.
 

 
 
 
 
 
 
 
 
 
No comments:
Post a Comment