RC wa Mbeya Mhe. Amos Makalla
akizungumza na wananchi huko Kapunga, Mbarali
RC Makalla apongeza hatua wanazochukua za kuboresha miundombinu ya umwagiliaji na kurejesha Maji mto Ruaha Mkuu
Azungumza na wakulima wadogo Kijiji cha Iyala na kuwaruhusu kutumia Maji japokuwa utumiaji hukufuata taratibu ila kwakuwa mazao yamebakiza mwezi mmoja na nusu Mkuu wa Mkoa na kamati ya makamu wa Rais wameridhia watumie na Msimu ujao watapewa utaratibu
Aidha, RC Makalla azindua mradi wa Maji kijiji cha Kapunga uliokarabatiwa kwa ufadhili wa Kampuni ya Kapunga Farm
Licha ya hayo yote, amezishukuru kampuni za Kapunga na Highland kwa kuchangia shughuli mbalimbali ktk jamii
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa huyo wa Mbeya ameiagiza Kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Mbarali kutoruhusu mifugo eneo tengefu la Ihefu.Aidha ameitaka Kamati ulinzi kufanya opresheni mara kwa mara na kufanya hivyo ni utekelezaji wa Tangazo la serikali la mwaka 2008 na wafugaji wote wakiondolewa eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune (wa kwanza mkono wa kulia) akiwasili eneo la Mkutano pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Amos Makalla (aliyevaa miwani)
Maendeleo kwa Vitendo
No comments:
Post a Comment