Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi Mgwatu,
ametembelea na kukagua kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola
na Ukara katika kisiwa cha Ukerewe mkoa wa Mwanza na kujionea utendaji kazi wa
kivuko hicho pamoja na changamoto zake.
Akiongea na watumishi wa kivuko hicho baada ya kujionea changamoto ya uendeshaji
wa kivuko hicho, Dkt. Mgwatu alisema “tutanunua injini mbili mpya na kukifanyia
matengezo ya kinga kivuko hiki ili kuongeza zaidi ufanisi wake na hatimae kiweze
kusafirisha abiria na mali zao kwa haraka zaidi na katika hali ya usalama mkubwa
kwani injini zilizoko sasa zimechoka hivyo kushindwa kuendesha kivuko ipasavyo.”
Aidha Dkt. Mgwatu aliwataka watumishi wa kivuko cha MV. Nyerere kufanya kazi kwa
bidii sambamba na kuziba mianya ya uvujaji wa mapato ya serikali, pamoja na
kuzingatia weledi na uadilifu katika utendaji wa kazi.
Katika hatua nyingine, Dkt. Mgwatu alitembelea kivuko cha MV. Mara katika Mkoa wa
Mara pamoja na kivuko cha MV. Ruvuvu katika mkoa wa Kagera na kujionea utendaji
kazi wa vivuko hivyo pamoja na changamoto zake.
Kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika
kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Fundi wa kivuko cha MV. Nyerere akionyesha utendaji wa injini mojawapo ya
kivuko cha MV. Nyerere kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika
kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza. Nyuma yake ni Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Iddi Mgwatu.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Iddi
Mgwatu (wa pili kushoto) akiangalia utendaji kazi wa moja ya injini ya kivuko
cha MV. Nyerere katika chumba cha mifumo ya kuendeshea kivuko hicho.
Kivuko cha MV. Nyerere kinatoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika kisiwa
cha Ukerewe mkoani Mwanza.
Kivuko cha MV. Mara kinachotoa huduma kati ya Iramba na Majita mkoani Mara.
Kivuko cha MV. Ruvuvu kinachotoa huduma katika eneo la Rusumo Mkoani
Kagera. Picha na Theresia Mwami.
No comments:
Post a Comment