Wafanyakazi wa Benki ya Wanawake Tawi la Mkwepu wameungana na Taifa kuombolea vifo vya wanafunzi 32, walimu 2 na dereva mmoja vilivyotokana na ajali iliyotokea Karatu mkoani Arusha tarehe 6 May, mwaka huu.
Kwa niaba Benki ya Wanawake wametuma salamu za pole kwa wazazi, walezi, familia na jamii yote ya Arusha na Tanzania kwa ujumla, kwa kupoteza watoto wetu ambao walikuwa waliokuwa wanandaliwa kuwa nguvu kazi ya Taifa letu katika Sekta mbalimbali.
Mwenyezi Mungu awapatie Faraja na Moyo wa Subira katika kipindi hiki kigumu cha huzuni, uchungu na simanzi kwa familia za marehemu na Taifa kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment