Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linawashikiria watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi ambao walifanya matukio mawili tofauti ya uporaji katika maeneo ya Boko pamoja na Sinza jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Kamishina Simon Sirro amesema majambazi waliwanasa wakiwa katika uhalifu wa uporaji baadhi ya maduka ya Boko.
Kamishina Sirro amesema wakati polisi wakiwa katika operesheni walifika maeneo hayo kisha majambazi wakaanza kutupa risasi na polisi wakajibu na kuwapiga na wakaanguka ndipo waliweza kuwachukua kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo walifariki wakiwa wanapatiwa matibabu.
Wakati huo huo jeshi la polisi limewakamta watu wawili ambao walikuwa wanazalisha Konyagi bandia ya chupa. Watuhumiwa hao ni Bahati Steve pamoja na Vumilia Andrea na uchunguzi unaendelea dhidi yao.
Hata hivyo jeshi la polisi limeweza kukamata dawa za kulevya mbalimbali pamoja na pombe zilizo katika vifungashio vya plastiki (Viroba).
Pia Jeshi la Polisi limeweza kumnasa Askari Feki Lyanga Baruti ambaye amesema sare za jeshi hilo aliziiba kwa kaka yake na kasha kuvaa.
Baruti amesema alizivaa na kwenda sehemu mbalimbali na kisha askari wakaweza kumnasa akiwa katika mizunguko yake.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Kamishina Simon Sirro akizungumza na waandishi habari juu ya operesheni ya wiki moja iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Kamishina Simon Sirro akionyesha konyangi bandia walizozikamata katika operesheni leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akimuonyesha Askari Feki, Lyanga Baruti mbele ya waandishi habari juu ya jinsi alivyoiba sare za polisi za kaka yake na kuanza kukata mitaa katika jiji Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Kamishina Simon Sirro akionyesha magazine na risasi walizozikuta kwa majambazi waliofanya matukio ya ujambazi kwa wiki ya iliyopita.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam , Kamishina Simon Sirro akionyesha magari ya ambayo yameibiwa kwa watu leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment