Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
Profesa Adolf Mkenda amesema serikali inaweka mazingira bora kwa wafanyabiashara ili waweze kuendelea
katika kujenga uchumi.
Profesa Mkenda ameyasema hayo wakati wa mkutano wa
mfuko wa sekta binafsi nchini (TPSF), Mkenda amesema sekta binafsi
inahitajika katika sekta ya viwanda ili nchi iweze kufikia uchumi wa kati ikiwa
ni pamoja na kuongeza ajira kwa vijana.
Amesema kuwa masuala yote ambayo yanayohusu yaingizwe katika
kamati iliyoundwa ili kuweza kufanyiwa kazi kwa maandishi juu mazingira ya sekta
binafsi kufanya biashara na nchi ipate maendeleo.
Mkenda amesema kuwa
serikali inafanya jitihada kila namna ya jinsi kuwawezesha wafanyabiasha kuendesha biashara zao na changamoto ziwekwe katika maandishi katika
kuzifanyia kazi pamoja na kushauri.
Kwa upande wa wafanyabiashara wamesema mamlaka za udhibiti zinafanya kazi kama biashara
wakati kazi zao ni za utoaji wa huduma.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Alaska Tanzania, Jennifer Bash amesema watendaji wawasaidie
wafanyabiashara katika kupata huduma mbalimbali ili Tanzania iweze kukua kiuchumi kupita sekta binafsi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf Mkenda akizungumza katika mkutano wa sekta binafsi kujadili masuala mbalimbali ya biashara nchini leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Sekta Binafsi nchini (TPSF), Dk. Reginald Mengi akizungumza katika mkutano kujadili masuala ya biashara nchini leo.
Mjumbe wa bodi ya TPSF, Silvester Koka akichangia maada katika Mkutano wa sekta binafsi uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Alaska Tanzania, Jennifer Bash
akichangia maada katika Mkutano wa sekata binafsi nchini leo jijini Dar
es Salaam.
No comments:
Post a Comment