Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S. Kebwe akifungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, mjini Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S.Kebwe katika picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa TCAA baada ya kufungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, mjini Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S.Kebwe akibadilishana mawazo na Menejimenti ya TCAA baada ya ufunguzi mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, mjini Morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe S.Kebwe akiagana na Mkurugenzi Mkuu wa TCAA Bw.Hamza S.Johari baada ya kufungua mkutano wa Baraza la wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA ), uliofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu, jijini Morogoro.
Na Ally Changwila
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt, Kebwe Stephen Kebwe
ameipongeza Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kwa kufanikisha mchakato wa ununuzi wa Rada nne za
kuongozea ndege nchini, kutokana na Mamlaka kubana matumizi yake na hivyo
kupata fedha za kununulia mitambo hiyo.
Akizungumza wakati wa kufungua Baraza la wafanyakazi la
TCAA lililofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa la Magadu jijini,Morogoro, Dkt Kebwe
aliongeza kuwa Rada hizo nne zitaifanya Tanzania kuwa katika nafasi nzuri ya
ushindani katika sekta ya usafiri wa anga kwenye ukanda huu wa Afrika Mashariki
na Afrika kwa ujumla.
“Mafanikio yenu katika kuyafikia malengo yatategemea kila
mmoja wenu kutimiza wajibu wake kwa kadri ya uwezo wake”. Aliongeza.
Vile vile Dkt. Kebwe ameipongeza TCAA kwa mafanikio
iliyoyapata kwa kufaulu ukaguzi wa Shirika la kimataifa la Usafiri wa Anga-ICAO
kwa kufikia asilimia 61.
Dkt Kebwe ameongeza kuwa mafanikio ya TCAA ni mafanikio
ya sekta nyingine kwani sekta ya usafiri wa Anga ni kiungo muhimu cha
kuziwezesha sekta nyingine za uchumi kama utalii, kilimo na madini na kadhalika
kuendelea kukua.
Dkt Kebwe pia ameongeza, Usafiri wa Anga si usafiri wa
anasa bali ni usafiri wa msingi kwa kuchochea maendeleo, na kwamba Tanzania
inapaswa kufanya jitihada za kuongeza
watoa huduma za usafiri wa anga ikiwa ni pamoja na mashirika ya ndege
mengi kutoa fursa kwa wananchi wengi kuutumia usafiri huo kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment