Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Timu ya mpira wa wavu (Volleyball) ya wanawake ya Magereza imetwaa ubingwa wa mchezo huo katika mashindano ya Muungano yaliyofikia tamati jana katika uwanja wa Taifa wa Ndani jijini Dar es Salaam.
Timu ya Magereza ya wanawake licha ya kufungwa mchezo wao wa mwisho dhidi ya Jeshi Stars wanawake kwa seti 3-2 walifanikiwa kuibuka mabingwa kwa tofauti ya pointi.
Kwa upande wa wanaume, timu ya mpira wa wavu (Volleyball) Jeshi Stars wamefanikiwa kuibuka mabingwa wa mashindano ya Muungano baada ya kufanikiwa kuwafunga Magereza kwa ushindi wa seti 3-1.
Mabingwa hao wamekabidhiwa zawadi pamoja na kikombe na aliyekuwa mgeni rasmi Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Mohamed Kiganja.
Mchezaji wa timu ya mpira wa wavu (Volleyball) ya Jeshi Stars, Fordey Edward ameibuka mchezaji bora (MVP) wa mashindano ya Muungano yaliyofikia tamati jana.
Fordey ameiwezesha timu yake ya Jeshi Stars kutwaa taji hilo baada ya kuifunga timu ya Magereza katika mchezo huo wa fainali. Fordey ambaye ni mkazi wa mkoa wa Tabora pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya mchezo huo
Nahodha wa timu hiyo Averine Albert akikabidhiwa kikombe na Mgeni rasmi Ndg. Ahmed Kiganja ambaye ni katibu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Nahodha wa timu hiyo ya Jeshi Stars Abel Masunga akikabidhiwa kombe lao.
No comments:
Post a Comment