Tatizo la wimbo wa Taifa na dua katika mkutano wa baraza la madiwani wa mkoa wa jiji la Dar es Salaam umeweza kuzua mjadala kwa zaidi ya dakika kumi katikati ya mkutano huo.
Mjadala huo ambao uliibuliwa na mtoa hoja, Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea ambaye alitoa hoja ya kukiukwa kwa kanuni za uendeshwaji wa baraza hilo.
Mara baada ya kutoa hoja mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam,Sipora Liana alimuomba mwanasheria wa halmashauri kutoa ufafanuzi juu ya swala hili na kusema kuwa hakuna kitu kilichoharibika jambo ambalo lilipingwa vikali na madiwani wote.
Mara baada ya madiwani kumpinga mwanasheria huyo na Mstahiki meya waliamuliwa na madiwani hao kurudia kuimba wimbo wa taifa kisha kufuatiwa na dua jambo ambalo liliridhia kuanza kwa mkutano huo bila mgogoro.
Hoja nyingine aliyoibua kubenea ilikuwa ni kitendo cha kuanzishwa kwa mkutano huo bila ya akidi kutimia na kumlazimu kurudia tena kuhesabu watu ili kujiridhisha kuwa akidi imetimia.
Hata hivyo dakika chache baadae mkutano ulivyoanza ulikuwa kwa majibizano ya hoja mbalimbali ikiwemo juu ya namna uwasilishaji wa taarifa hiyo.
Hata hivyo baraza hilo lilimalizika kwa Meya wa jiji Isaya Mwita kuairisha mkutano mpaka kesho.
Mstahiki Meya wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa jiji
Mbunge wa Ubungo na Diwani wa Baraza la Madiwani wa Jiji la Dar es Salaam, Saed kubenea akizungumza wakati wa kikao cha baraza.
Diwani wa kata ya Kibonde Maji, Abdalah Mtinika akitoa hoja katika kikao cha baraza la Madiwani kilichafanyika katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam.
Mayor wa Halmashauri wa Manispaa ya Temeke, Abdalah Chaurembo akitoa hoja katika kikao cha baraza la Madiwani wa jiji la Dar es Salaam
Madiwani wakiwa katika kikao baraza la Madiwani wa jiji la Dar es Salaam katika ukumbi wa Karimjee
No comments:
Post a Comment