Mwandishi wa habari Mwandamizi kutoka Michuzi Blog , Humphrey Shao akiongea na wasanii na Waandishi wa habari katika jukwaa la sanaa lililoandaliwa na BASATA juu ya tatizo la Dawa za kulevya kwa wasanii wa kwanza kulia ni Snura Mushi na watatu kutoka kushoto ni Msanii wa Mizengwe Hemed maliyaga(Mkwere Original) na katibu mkuu wa basata , Godfrey Mwingereza .
Katibu mkuu wa BASATA, Godfrey Mwingereza akizungumza na wasanii na waandishi habari juu ya kujikwamua katika tatizo la dawa za kulevya
wadau wa wasanaa na waandishi wa habari wakifatilia
Katibu mkuu wa Baraza la Sanaa Basata akizungumza na wasanii wa filamiu na muziki kabla ya kuingiakatika mkutano.
Na Ripota wa
globu ya jamii
Wito
umetolewa kwa wasanii kuacha kutumia dawa za kulevya na vileo kabla ya kuanza
kufanya kazi zao hili waweze kuongeza weledi wa sanaa kwa hadhira.
Wito huo umetolewa
na mwandishi mwandamizi wa Michuzi blog Humphrey Shao, alipokuwa akizungumza na
wasanii pamoja na waandishi wa habari katika jukwaa la Sanaa lililoandaliwa na
Baraza la Sanaa Tanzania(BASATA)
Akizungumza katika
jukwaa hilo Shao amesema kuwa ameweza kuandika makala nyingi sana zinazousu
matatizo ya dawa za kulevya kwa wasani tangu mwaka 2014 lakini mwaka huu 2017
ndipo mambo yote yamekuwa hadharani.
“tatizo la
dawa za kulevya kwa wasanii alijaanza leo na wengi wao uanzia na kilevi cha
bangi na kupelekea kujingiza kwenye dawa za kulevya hali inayo hatarisha maisha
yao na kazi zao za sanaa”amesema Shao.
Kwa upande
wake msanii wa muziki wa Bongo Fleva Snura Mushi amesema kuwa amekuwa
akishuhudia wasanii wengi ambao awawezi kupanda jukwaani mpaka walewe hali
inayopelekea wengi wao kuharibu kazi na kupoteza mashabiki.
Ametaja kuwa
mtu ukitumia madawa yakulevya au pombe katika kazi yako inakufanya upoteze
umakini ambao unaweza kukupoteza katika ramani ya sanaa na heshima yako
kushuka.
Nae katibu
mkuu wa BASATA, Godfrey Mwingereza ametoa onyo kwa wasanii wote ambao wanatumia
dawa za kulevya na wale upendelea kunywa pombe kupita kiasi na kupanda katika
majukwaa ya muziki.
Mwingereza
amesema kuwa kitendo cha msanii kupanda jukwaani akiwa amelewa ni kudhalilisha
kazi ya sanaa ambayo ni kazi kama ilivyo kazi nyingine na kutaja kuwa ni mara
chache sana kuona wakandarasi au madaktari kuona wakiwa katika kazi zao
wamelewa kama wasanii wetu.
No comments:
Post a Comment