Na Yassir Adam, Globu ya Jamii
Tanzania ni moja kati ya nchi za Jumuiya yaAfrika mashariki ambayo haijaondoa vikwazo vya Kiforodha jambo linalowakwamisha Wananchi kufanya biashara katika Soko la Afrika Mashariki.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Mkurungezi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi TPSF Godfrey Simbeye amesema utekelezaji wa vikwazo hivyo utawasaidia wananchi kufanya biashara kutoka sehemu moja hadi nyingine.
"bado hatujapiga hatua ya kutosha ya kuondoa vikwazo visivyo vya Kiforodha ambapo Tanzania haijatekeleza kwa asilimia 27 tofauti na Kenya kwa asilimia 24 pamoja na Uganda kwa asilimia 15."
Simbeye amesema sheria mbalimbali zilizopo zinatakiwa zibadilishwa ili kufungua na kupunguza vikwazo vya ufanyaji wa biashara ili kupunguza vikwazo na kufikia Soko Afrika Mashariki.
"vikwazo vingi vilivyopo ni ucheleweshaji usiokuwa wa lazima katika Mizani,taratibu za forodha zenye usumbufu pamoja na kuwepo kwa Mifumo tofauti ya kutoa vibali,Ukaguzi na Upimaji."
Kwa upande wake Afisa Biashara kutoka Wizara ya Viwanda ,Biashara na Uwekezaji Fredy Kavula akaeleza kuwa lengo kubwa la kuondoa Vikwazo katika biashara ni kurahisisha biashara za Ndani na Nje kuvuka Mipaka na kufikia Soko la SADC na pia kufikia Mikataba ya Shirika la biashara la Dunia WTO.
"Wizara kwa kushirikiana na Kamati ya Kitaifa ya kusimamia na kuondoa vikwazo vya biashara imeweza kuondoa Vikwazo 114 na vilivyobakia ni 19 ambavyo bado kamati inavifanyia kazi kupitia Taasisi yenye Wajumbe wa kamati husika iliyojumuisha Taasisi binafsi pamoja na Serikali vitakavyorahisisha Biashara za ndani na nje kuvuka Mipaka"
Mkurugenzi Mtendaji Godfrey Simbeye akizungumza na waandishi wa Habari katika Mkutano huo uliohusu Uondoaji wa Vikwazo vya Kiforodha vya kibiashara Nchini
Baadhi ya Wadau mbalimbali kutoka serikalini na Sekta Binafsi waliohudhulia katika mkutano huo
No comments:
Post a Comment