Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akionesha mfano wa Taa zinazotumia mionzi ya jua ambazo vijana 20 katika Kata ya Nyegina watafundishwa namna ya kuzitengeneza baada ya kuzindua mafunzo hayo. Kulia ni Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung na kushoto ni Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi.
Mkufunzi wa mafunzo ya kutengeneza Taa na Chaja zinazotumia mionzi ya jua, Dkt. Dkt. Hong- Kyu Choi, akiwaleza washiriki wa mafunzo namna mafunzo hayo yatakavyoendeshwa.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Dkt. Vicent Naano, (wa tatu kushoto) akiongea jambo mara baada ya uzinduzi wa mafunzo ya Kutengeneza taa na chaja zinazotumia mionzi ya jua. Wengine ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muongo (katikati), Balozi wa Korea Kusini nchini,Song Geumyoung Mkufunzi wa mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi (wa pili kulia) na baadhi ya wawakilishi wa vijana wanaoshiriki mafunzo.
Mtaalam kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Emmanuel Yesaya, akizungumza jambo kuhusu utekelezaji wa REA awamu ya Pili na ya Tatu, katika Kata hiyo wakati wa Mkutano wa Waziri wa Nishati na Madini (hayupo pichani) na wananchi wa Kata ya Nyegina.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) akikagua vitabu ambavyo baadhi alivigawa katika katika Kituo cha Sekondari ya Nyegina katika shule mbalimbali Mkoani Mara. Kulia ni Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Nyegina na Paroko wa Parokia hiyo, Padri Leo Kazeri.
Balozi wa Korea Kusini nchini,Song Geumyoung (wa tatu kulia) akiwa ameshika Taa za mfano ambazo vijana 20 kutoka Kata ya Nyegina watapewa mafunzo ya namna ya kuzitengeneza. Wengine wanaofuatilia ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Vijijini Dkt. Vicent Naano,(wa tatu kushoto) Mkufunzi wa Mafunzo hayo, Dkt. Hong-Kyu Choi (wa pili kushoto) na wawakilishi wa mafunzo hayo.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akiweka tofali katika moja ya vyumba vya madarasa vinavyojengwa katika Shule ya Msingi Kata ya Bwasi, wakati wa ziara yake ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo. Wengine ni Viongozi wa Vijiji, Halmashauri na wananchi wa Kijiji cha Kome.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (mwenye tisheti nyeusi) akiongea na wanafunzi wa shule ya msingi ya Kome mara baada ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa na kuongea na wananchi wa Kijiji hicho.
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akimsikiliza mmoja wa wananchi aliyehudhuria katika mkutano wa Waziri na Wananchi wa Kijiji cha Kome. Wengine ni wanafunzi wa Shule ya Msingi wa Kome.
Waziri wa Nishati na
Madini ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Profesa Sospeter
Muhongo amezindua Mafunzo ya namna ya
Kutengeneneza Taa na Chaja zinazotumia mwanga wa jua kwa vijana 20 katika Kata ya Nyegina Mkoa wa Mara.
Akifungua mafuzo hayo
Profesa Muhongo amewataka vijana hao kuwa mabalozi wazuri wakati wanapohudhuria
mafunzo na kueleza kuwa, yatakuwa chachu katika kupanua wigo wa wa ajira ikiwemo wahitimu kujiari wenyewe.
Profesa Muhongo
amewataka vijana na wananchi mkoani humo kuweka nguvu kubwa katika elimu
kutokana na umuhimu na mchango wake kwa
maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
Akizungumzia kuhusu
Mradi wa Usambazaji Vijijini Awamu ya Tatu, Profesa Muhongo ameeleza kuwa,
awamu hiyo itaanza kutekelezwa kuanzia mwezi Machi mwaka huu na kuongeza kuwa,
mradi huo utafanywa kwa Awamu na kusisitisza kuwa, adhma ya Serikali ni
kuhakikisha kuwa, ndani ya kipindi cha miaka mitano vijiji vyote nchini viwe
vimeunganishwa na nishati hiyo.
" Vijiji vyote
vitaunganishwa na nishati ya umeme. Tutasambaza
awamu kwa awamu na lengo letu ni kuhakikisha kuwa, vijiji vyote chini
vinaunganishwa na umeme ndani ya kipindi cha miaka mitano. Wale ambao
hawajafikiwa awamu ya kwanza na ya pili tutawafikia awamu ya tatu vivyo hivyo
mpaka tufikie lengo letu," amesisitiza Prof. Muhongo.
Kwa upande wake
Balozi wa Korea Kusini nchini, Song Geumyoung ambaye nchi yake imefadhili
mafunzo hayo, amesema kuwa, uwepo wa taa
hizo utasaidia upungufu wa umeme hususan maeneo ya vijijini na ambayo bado
hayajaunganishwa na nishati hiyo.
Aidha, amesema kuwa,
mafunzo hayo ni fursa ya ajira kwa wahitimu watakaopata mafunzo hayo ikiwemo
nafasi za kuajiriwa na hivyo kuwataka kutilia mkazo mafunzo hayo na kueleza
kuwa, mafunzo hayo ni mwanga kwa vijana.
Aidha, ameongeza
kuwa, kutokana na urafiki wa miaka mingi
baina ya nchi za Tanzania nasini , hirikinchi hiyo itlea kushirikiana na
Tanzania kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na umeme wa uhakika.
"Kama ilivyo kwa
kaulimbi ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt.
John Magufuli, Hapa Kazi Tu' na mimi napenda kusema tusiende polepole twende
'Haraka, Haraka", amesisitiza Balozi
Geumyoung.
Kwa mujibu wa
Professa Muhongo mafunzo hayo yanatarajiwa pia kutolewa katika Kata za Mwirangi, Bukima na Mgango.
Naye Mkufunzi wa Mafunzo hayo Dkt. Hong- Kyu Choi, amesema kuwa, baada ya
kuzifikia Kata zote zilizoainishwa, watachaguliwa wanafunzi bora ambao watakuwa
mabalozi wa mafunzo hayo na hivyo kuwataka washiriki wa mafunzo hayo kufuatilia
mafunzo hayo na kuyachukulia kwa uzito mkubwa.
Mbali na kufungua
mafunzo hayo, Profesa Muhongo pia amekagua miradi ya umeme Awamu ya Pili
inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na kukagua ujenzi wa
vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Kome katika kijiji cha Kome, Kata ya
Bwasi. Mafunzo hayo
yamezinduliwa tarehe 20 Februari,2017
No comments:
Post a Comment