Timu ya Mwandege kutoka kata ya mwandege na Lukanga fc kutoka kata ya Lukanga zimefanikiwa kuingia hatua ya Nusu fainali baada ya kuzisambaratisha timu ya Mkamba ya kata ya mkamba pamoja na timu ya Mbezi fc ya kata ya Mbezi.
Katika mechi ya kwanza, timu ya Mkamba ndio iliyotangulia kufunga timu ya Mwandege katika kipindi cha kwanza bao lililofungwa na ,Abdallah Matope na hadi wanakwenda mapimziko Mkamba walikuwa wanaongoza kwa bao moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu hizo kushambuliana kwa zamu ambapo katika dakika ya 15 ya kipindi hicho timu ya Mwandege walisawazisha goli kupitia Salumu Mnyasi waliendelea kushambuliana lakini Mwandege walionekana kutakata zaidi ambapo dakika ya 25 Mussa Charles aliipatia Mwandege FC goli la pili.
Hadi dakika 90 zinamalizika Mwandege waliibuka na ushindi wa goli 2-1 na kutinga nusu fainali.
Katika mechi ya pili Lukanga FC ilifanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga timu ya Mbezi kwa goli 3-0 yote yakifungwa kipindi cha pili.
Mchezo huo ulishuhudiwa na watazamaji wengi wakiongozwa na mheshimiwa Mbunge,Abdallah Hamis Ulega.
Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa anashuhudia moja ya mtanange wa kombe la Ulega Cup linaloendelea Wilaya ya Mkuranga.
Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa Mwandege na Mkamba FC katika mashindano ya Ulega CUP mchezo uliopigwa jana.
Wachezjai wa Mwandege Fc wakipambana na wachezaji wa Mkamba Fc kwenye mchezo wa robo fainali uliofanyika jana, Mwandenge walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 2-1.
No comments:
Post a Comment