Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya makabidhiano hayo eneo la Kisarawe II wilaya ya Kigamboni leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Masaka.
Na Benjamin Sawe
Sekta ya Viwanda na Biashara hutoa ajira kwa
asilimia 62 ya wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Mkoa wa Dar
es Salaam una jumla ya wakazi 4,364,541 kati yao watu wenye umri wa kufanya
kazi (miaka 15 -
64) ni asilimia 66.3 (2,893,691); wengi wao wanafanya kazi za biashara na ajira
viwandani.
Awali Tanzania iliweza kutoa ajira kwa vijana
wengi kupitia viwanda vyake vya nguo vilivyokuwa katika mikoa mbalimbali kama
kile cha Urafiki cha Dar es Salaam na vinginevyo ambavyo hata hivyo kwa sasa
viko hoi kutokana na kuhujumiwa na watendaji wasio waaminifu.
Sekta ya viwanda ni sehemu muhimu katika uchumi wa
Taifa. Mkoa wa Dar es Salaam una viwanda vingi vya aina mbalimbali kufuatana na
bidhaa zinazozalishwa.
Katika Mkoa wa Dar es Salaam kuna bidhaa za aina
mbalimbali pamoja na huduma zinazouzwa kwa kiwango kikubwa na kupelekwa nje ya
Mkoa.
Bidhaa hizo ni pamoja na zinazozalishwa katika
viwanda viliyopo hapa Mkoani na zile zinazoagizwa toka nje ya nchi.
Tanzania haiwezi kubadilika ikiwa mawazo ya watu
hayatabadilika katika ujenzi wa viwanda vidogo nchini kote na kuondoa mawazo ya
kujenga viwanda vikubwa kama vya wafanyanyabiashara wakubwa, kwa kuwa
vinahitaji mtaji mkubwa wakati ajira zake ni chache.
Ama
kwa hakika kila mmoja wetu anaifahamu dira na dhamira ya serikali ya awamu ya
tano ya Dr. John Pombe Magufuli ya kuifuta historia yetu ya aibu ya muda mrefu
ya kuwa na taifa la wachuuzi kwa kuligeuza kuwa taifa la wazalishaji kupitia
kuchochea uanzishwaji wa viwanda vya kutosha chini ya mwamvuli wa sera ya
Tanzania ya viwanda.
Ni kwasababu hiyo tu, watendaji wake aliowaamini na kuwapa dhamana, hawana budi kuendelea kuwaza zaidi,
kutenda zaidi na kushirikisha washirika wengi zaidi ili kwa pamoja waikamilishe
ndoto hii ya Rais wetu mpendwa.
Ushirikiano baina ya Makonda na Azimio Housing Estate kampuni ambayo
imekubali kutoa eneo lililopo Kigamboni
lenye ukubwa wa ekari 1500 la thamani ya zaidi ya bilioni 121 na milioni 470
litakalotumika kama eneo maalumu mbalo litagawiwa kwa wajasiriamali zaidi ya
3,000 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo ni mfano wa kuigwa na kupongezwa
kwani hii inaonyesha wazi dhamira ya Mheshimiwa Makonda ya kuwakomboa
wajasiriamali wadogo wa jiji la Dar es Salaam.
Pamoja
na mambo mengineyo mpango huo unakusudia kuwasaidia wamiliki wa viwanda vidogo
kupata maeneo yao ya kufanyia kazi ili kuwapunguzia gharama za kukodi maeneo,
kuwaepusha na usumbufu wa kukaa maeneo yasiyo rasmi pamoja na kuwapatia uhakika
wa kuwa na anuani (address) za kudumu.
Kutokana
na kauli ya Mheshimiwa Makonda kuna matumaini kwamba neema inawajia wanadar es
salaam ya ajira na soko la bidhaa zao kutokana na ujio wa viwanda hivyo.
Watu
wenye viwanda vidogo wana changamoto nyingi za maeneo na wengine kulazimika
kuweka katika maeneo ya watu na kusababisha kero kwa wananchi wanaoishi karibu
na maeneo hayo.
Kwa
ujumla, ujenzi wa viwanda si kitu kidogo, unahitaji muda na rasilimali nyingine
nyingi kufanikisha hatua inayotarajiwa na umma.
Ndoto
ya Tanzania kuwa nchi ya viwanda, inaelekea kutimia baada ya Serikali ya Awamu
ya Tano kuonesha kwa vitendo dhamira yake ya kuhakikisha ndoto hiyo inatimia.
Mnyonge
mnyongeni haki yake mpeni. Paul Makonda anastahili pongezi kubwa na za dhati
kabisa kwa mkakati wake wa kujenga Dar es Salaam mpya.
No comments:
Post a Comment