HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 4, 2017

DK.SHEIN AWAANDALIA CHAKULA MAASKARI WALIOSHIRIKI GWARIDE LA MAADHIMISHO YA MIAKA 53 YA MAPINDUZI.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia mkono maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar wakati alipowasili katika hafla ya chakula maalum kwa Askari hao iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni (kulia) Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman ,Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akiwa na Viongozi mbali mbali wakisimama wakati Wimbo wa Taifa ukipigwa wakati wa hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya kuwasili katika hafla hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiteta jambo na Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman wakati wa hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar mara baada ya kuwasili katika hafla hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, (wa pili kushoto) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ Haji Omar Kheir,(kushoto) Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid na Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman (wa pili kulia) wakiwa katika hafla ya chakula maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akichukua chakula wakati wa hafla ya chakula maalum iliyoandaliwa kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.
 Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, (wa pili kushoto) na Kamanda wa Brigedia ya Nyuki Zanzibar Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman (wa pili kulia) wakichukua chakula katika hafla maalum kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, hafla hiyo iliyofanyika leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni.
 Maaskari wa vikozi vya ulinzi walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar
 /Maaskari wa vikozi vya ulinzi walioshiriki sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,wakichukua chakula cha mchana kilichotayarishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein leo katika viwanja vya Kambi ya KVZ Mtoni Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiagana na Brigedia Jeneral Sharif Sheikh Othman,Kamanda wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar baada ya hafla ya Chakula maalum aliyoiandaa kwa maaskari walioshiriki katika sherehe za Maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,Sherehe iliyofanyika leo katika kambi ya KVZ Mtoni Mkoa wa Magharibi Unguja.
PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad