Raisi wa klabu ya Simba Evance Aveva
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Raisi wa klabu ya Simba Evance Aveva amewataka wanachama 71 wa klabu hiyo waliofungiwa kushiriki shughuli mbalimbali za klabu hiyo kutokana na kosa la kupeleka mahakamani masuala ya soka, kwenda kuifuta kesi hiyo mahakamani ili waweze kuruhusiwa kuendelea kuwa wanachama halali.
Aveva aliyasema hayo wakati wakizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam, kitendo kilichofanywa na wanachama hao kilikuwa na kinyume na katiba ya klabu hiyo, TFF pamoja na katiba ya FIFA, hivyo kupelekea kamati tendaji kwa pamoja kuchukua maamuzi ya kuwafungia ili kuwakumbusha kanuni wanachama wa klabu hiyo ambao walikuwa na lengo la kufanya kama walivyofanya wao.
"Kila mmoja natumaini sio mgeni wa kanuni zinazoendesha soka letu na tumeamua kuchukua maamuzi ya kuwataka wafute shitaka walilolifungua ili warudi kundini kwa sababu tumetambua ili tufanye vyema ni lazima tuwe na umoja na mshikamano kwani bila hivyo kupata mafanikio ni vigumu," alisema Aveva.
Wakati wa uongoozi wa Rais huyo wakiingia madarakani wanachama 71 waliamua kufungua kesi mahakamani na kwenye mkutano mkuu wa wanachama kwa pamoja walikubaliana kuwavua uanachama.
Aveva alisisitiza kuwa katika kuijenga Simba, wanachama kwa pamoja wanatakiwa kuwa wamoja na kushirikiana kuhakikisha inasimamia malengo na mikakati ya klabu hiyo.
No comments:
Post a Comment