Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisaini daftari la wageni baada ya kuwasili wilayani Momba Mkoani Songwe, kwa lengo la kutembelea na kukagua uingiaji na utoakaji wa raia na wageni katika mpaka wa Tunduma unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Afisa Uhamiaji Mpaka wa Tunduma akimuelekeza jambo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), wakati wa ziara ya kutembelea mpaka huo unaotoa huduma kwa watu wanaoingia na kutoka katika nchi za Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afika Kusini, Namibia na DRC Congo.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando akizungumza na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, walipotembelea jiwe (linaloonekana pichani) linalotenganisha nchi ya Tanzania na Zambia.Wengine ni Wakuu wa Idara za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto na Polisi walioambatana na Naibu Waziri katika ziara hiyo mkoani Songwe.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mpakani Tunduma huku akiwaasa kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa wahamiaji haramu wanaoingia nchini kupitia mpaka huo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni (wanne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa
Serikali na Wakuu wa Idara za Uhamiaji, Magereza, Zimamoto, Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) na Polisi baada ya kutembelea mpaka wa
Tunduma.Ambapo aliwaasa kushirikiana kwa pamoja katika kudhibiti uingiaji wa
wahamiaji haramu wanaoingia nchini
kupitia mpaka huo. Wapili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Momba, Juma Irando.
IMEANDALIWA
NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
No comments:
Post a Comment