HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 20, 2017

YANGA TAYARI KUIVAA ASHANTI UNITED KOMBE LA FA KESHO

Kikosi cha Yanga

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mabingwa watetezi wa kombe la Shirikisho FA Yanga wanatarajiwa kushuka dimbani kesho kupambana na wauza mitumba wa Ilala Ashanti  United katika mchezo wa hatua ya 32 ya kombe hilo ikiwa ni raundi ya Tano toka kuanza kwa msimu wa pili wa mashindano hayo.

Kikosi hicho cha Mzambia George Lwandamina, kikiwa kimetoka kupata ushindi wa ugenini dhidi ya Majimaji ya Songea watashuka  katika Uwanja uhuru kuhakikisha wanaendeleza kutetea ubingwa wao huku wakiwakosa nyota wao kadhaa.

Akizungumza na globu hii, Kocha msaidizi Juma Mwambusi amesema kuwa kikosi chake kimejianda kikamilifu kwa ajili ya kutoka na ushindi na wana matumaini  na vijana wao kwani   watajituma kulingana na maelezo waliyowafundisha ili kutetea kombe hilo.

"wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri huku wakiwa na morali ya kushinda ili kujiweka kwenye mazingira  mazuri katika michuano na kuendelea kulitetea kombe letu hata hivyo katika mchezo wa kesho tutawakosa nyota wetu kadhaa ambao bado ni majeruhi lakini Donald Ngoma hatakuwepo kwakuwa amefiwa na kaka yake na amesafiri kwenda nchini Zimbabwe, "amesema Mwambusi.

Wachezaji watakaowakosa katika mchezo huo ni  Donald Ngoma,Obbey Chirwa, Justin Zullu na ,Vicent Bossou anayeitumika timu yake ya Taifa ya Togo.

Emauel Martin na Malimi Busungu wameungana na wachezaji wenzao kwenye mazoeezi ya leo kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Ashanti.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad