Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Msajili wa Baraza la Famansia nchini, Elizabeth Shekalaghe amesema maduka yote ya famasi yanatakiwa kuwa na mtaalam wa famasia.
Akizungumza katika semina ya utoaji leseni kwa wafamasia pamoja na miongozo, amesema wafamasia wanafanya kazi za maisha ya binadamu hivyo kuwa na duka la famasi bila kuwa fani ya famasia ni kosa kisheria.
Elizabeth amesema wafamasia lazima wafanye kazi kwa maadili yaliyowekwa na watakaokwenda kinyume baraza hilo litachukua hatua.
Elizabeth amesema kwa sasa nchi hii inapoelekea kwenye sera ya Viwanda ni fursa kwa wafamasia kuungana kwa kuwa kiwanda cha kuzalisha dawa.
Aidha amesema sheria inataka kila duka la famasi kuwa na mfamasia mmoja. Amesema soko la wafamasia ni kubwa hivyo wanahumuimu sana serikalini pamoja sekta binafsi. Elizabeth amesema mwaka 2013 walikuwa na wafamasia 350 na kufikia mwaka jana wamefikia wafamasia 1400.
Msajili wa baraza la Famasia, Elizabeth Shekalaghe akizungumza katika semina ya kuwajengea uwezo wafamsia iliyofanyika ukumbi wa. TFDA ,jijini Dar es Salaam.
Wafamasia wakila kiapo
Sehemu ya wafamasia wakiwa katika semina.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii .
No comments:
Post a Comment