HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 16, 2017

SENEGAL YAWA TIMU YA KWANZA KUPATA USHINDI MICHUANO YA AFCON 2017


Na Bakari Issa Madjeshi
Timu ya Taifa ya Senegal maarufu kama Simba wa Teranga hatimaye imekuwa timu ya kwanza kupata ushindi katika mfululizo wa mechi za hatua ya makundi ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa mwaka 2017.

Senegal inayoshiriki michuano hiyo inayoendelea nchini Gabon imefanikiwa kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Tunisia ikiwa ni mchezo wa kundi B ambapo kabla yake kulitanguliwa kwa mchezo wa kundi hilo baina ya Algeria dhidi ya Zimbabwe ambao walitoka sare ya bao 2-2.

Katika mchezo huo,Senegal ilifanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia mkwaju wa penalti uliokwamishwa wavuni na Mshambuliaji anaeichezea Liverpool ya Uingereza,Sadio Mane baada ya Kiungo wake,Cheikhou Kouyate kuangushwa katika eneo la hatari.

Dakika 30 ya mchezo,Simba wa Teranga walipachika bao la pili kupitia kwa Mlinzi wake,Kara Mbodji baada yakumalizia mpira uliokufa uliopigwa na .

Licha ya mabao hayo kupatikana katika Kipindi cha kwanza,Tunisia walionekana kuja juu zaidi kipindi cha pili kutaka kusawazisha mabao hayo lakini mbinu zao hazikiwezekana.

Hata hivyo mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika,Senegal waliweza kutoka kifua mbele kwa mabao yake 2-0 dhidi ya Waarabu hao.

Tangu kufunguliwa kwa michuano hiyo Januari 14 michezo ya kundi A ilifanyika kwa wenyeji,Gabon kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Guinea Bissau kabla ya Cameroon kwenda sare ya 1-1 pia na Bukina Faso 'Wabukinabe'

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad