Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Mh.Amos Makalla amekagua ukamilishaji wa madarasa kwa wanafunzi 406 waliokuwa wamekwama kuanza masomo kutokana na upungufu wa Madarasa
Kati ya wanafunzi 406 walikosa nafasi kuanza masomo ni 192 madarasa yao yamekamilika na wanafunzi 214 madarasa yao yatakamilika katika siku 14
Hivyo ili wanafunzi 214 wasiendelee kuchelewa ameridhia na kuagiza maabara ambazo zipo na hazijaanza kutumika kwa kukosa Vifaa sasa zitumike kama madarasa kuanzia jumatatu na baada ya madarasa kukamilika tarehe 30 januari wanafunzi hao watatumia madarasa hayo.
Rc.Makalla amezipongeza halmashauri za jiji la Mbeya na Mbeya vijijini kwa kuchangia ukamilishaji madarasa na amewashukuru wananchi na wadau kwa kuchangia ujenzi wa madarasa.

No comments:
Post a Comment