Baadhi ya watendaji wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakiwasili mkoani Morogoro, kuhudhuria mkutano mkuu wa nane wa chama hicho utakaofanyia kwa muda wa siku mbili na kuwashirikisha watendaji na wawakilishi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mororgoro (ACP) Leonce Rwegasila (katikati), akipokea taarifa ya washiriki wa mkutano mkuu wa nane wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), kutoka kwa (ASP) Emmanuel Katabi, kulia ni Meneja Mkuu wa URA SACCOS (SSP) Kim O. Mwemfula, na wamwisho ni (ASP) Bakari H. Mzungu.
Mwezeshaji Mkaguzi wa Polisi (INSP) Edwin B. Mkole , akiwasilisha mada kuhusiana na taratibu za utoaji wa mikopo kwa wanachama wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), wakati wa mkutano mkuu wa nane wa chama hicho unaofanyika mkoani Morogoro.
Kaimu kamanda wa Polisi mkoa wa Mororgoro (ACP) Leonce
Rwegasila (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji
wa chama cha ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha
Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), mara baada ya ufunguzi wa mkutano mkuu
wa nane unaofanyika mkoani Morogoro.
(Picha zote na Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi)
Na
Demetrius Njimbwi – Jeshi la Polisi Morogoro
Jeshi la Polisi nchini, limeendesha
mafunzo ya kuwajengea uwezo watendaji wa chama cha
ushirika cha kuweka akiba na kukopa cha Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD)
ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wanachama wao kote nchini huku ikiweka
dhamira ya kutoza riba ya mkopo kwa asilimia
10.5 kwa mwaka.
Akifungua mafunzo
ya siku mbili yanayofanyika mkoani Morogoro, Kaimu kamanda wa Polisi hapa (ACP)
Leonce Rwegasila, alisema kuwa, kwa kuzingatia umuhimu na uzito wa mkutano huu
ni vyema kila mshiriki akazingatia mahudhui ya kile kitakachotolewa ili kuwa
mjumbe mzuri kwa kupeleka elimu mahala alikotoka, alisema.
Hata hivyo,
alisema, katika mafunzo haya zipo mada pamoja na mijadala mbalimbali itakayojadiliwa
ili kuja na majibu mujarabu yatakayowezesha kuwa na Saccos imara na yenye
kukidhi mahitaji kwa wanachama wao ambao
ni askari Polisi pamoja na familia zao.
Kwa upande wake Meneja Mkuu wa URA SACCOS LTD (SSP) Kim O.
Mwemfula, alisema zipo huduma zilizoanzishwa za uhakika za ushirika wa
kuweka akiba na kukopa kupitia Usalama wa Raia Saccos (URA SACCOS LTD), ambapo
askari aliye mwanachama wa ushirika huo uweza kuweka na kukopa kwa riba nafuu
ili kuweza kuboresha maisha yake na familia yake katika Nyanja za Kielimu,
Biashara na hata Ujenzi wa nyumba.
Ameongeza kuwa, masuala ya ustawi
kwa askari yamesaidia kujenga utulivu wa akili kwa askari Polisi pamoja na
kuboresha suala la ustawi wa usalama wa raia na mali zao na kulifanya taifa
kuwa la amani na utulivu na kukabiliana na aina zote za matishio ya kiuhalifu
na wahalifu.
No comments:
Post a Comment