Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
BARAZA la Vyama vya Siasa nchini limesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano sasa inatekeleza mnyumbuliko wa uwajibikaji wa utawala bora kwa maendeleo ya Jamii na Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo , John Shibuda amesema uwajibikaji kumechangia ustawi na maendeleo ya nchi pamoja na uishi na uhai wa vyama vya kisiasa katika sekta ya utawala bora wa awamu ya tano.
Amesema kutokea kwa mawimbi ya kisiasa na kutokea kwa tetemeko la kuyumba kwa uthabiti wa uishi na uhai wa kazi za Siasa nje ya vyama na ndani ya Umma, katika mwaka 2016.
Baraza la vyama vya Siasa Tanzania, limemtakia heri Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na viongozi wake wasaidizi wakuu ambao ni Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu, Waziri Mkuu, Majaliwa Kassim Majaliwa na viongozi wote waambatana na Serikali ya awamu ya Tano.
Shibuda amesema utumishi wa Serikali kwani wanaonufaika ni Jamii na Taifa na furaha ya mwanasiasa aitwaye ni maslahi Jamii na Taifa inapaswa kushangilia uokovu unaotekelezwa na Serikali ya awamu ya tano.
Amesema Serikali ya awamu ya tano wamenufaisha Jamii na Taifa ambapo ndio yalikuwa hasa yanasumbua vyama vya Siasa vya upinzani katika awamu za serikali zilizopita.
“Kwa umuhimu wa pekee napenda kufichua angalizo la kwamba,Tanzania ya Serikali ya awamu ya Tano tuipongeze imetekeleza uvumbuzi ambao umekuwa ni tabibu kwa kasoro zilizokuwa ni hitilafu kwa Serikali ya CCM kuitwa ni Serikali ya watu wa Tanzania waliokombolewa na TANU na ASP” amesema Shibuda.
Amesema kulikuwa na kasoro zilizokuwa na hitilafu ambazo awamu ya Tano imedhibiti mirija ya unyonywaji wa pato la Taifa wa kupitia watumishi hewa, wanafunzi hewa, kaya za masikini Bandia na kupitia wahujumu uchumi wa matumizi mabaya ya dhamana za Taifa.
Shibuda amesema Serikali ya awamu ya Tano imerejesha uhodari, uwajibikaji wa watumishi na sasa wamekuwa wana tabia za miiko ya utiifu kwa Umma.
Amesemai sasa urasimu katika utolewaji wa huduma kwa mahitaji ya ustawi wa maendeleo ya Jamii ya Afya na Elimu na utatuzi wa kero kwa kasi ya kuwepo uishi wa Amani na furaha kwa makundi yote ya kijamii.
Aliongeza kuwa uhuru wa nchi sasa umekuwa siyo wa kunufaisha tabaka maalum la Raia wa Tanzania ni watu wote wamekuwa wanufaika na uhuru wao katika nchi na maendeleo yanaonekana.
Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala mbalimbali ya baraza hilo pamoja na kutakia heri ya mwaka huu leo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Msajili Msaidizi wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Sisty Nyahoza na kushoto ni Mjumbe wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini,Juma Ali Khatib.
Waandishi wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Nchini, John Shibuda leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
No comments:
Post a Comment