HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, January 26, 2017

MMILIKI MWENZA WA JAMII FORUM APANDISHWA KIZIMBANI

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mmiliki mwenza wa kampuni ya Jamii Media, Mike Mushi amefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kuunganishwa katika mashtaka yanayomkabili mkurugenzi wa kampuni hiyo Maxence Melo.
Washtakiwa wote wawili walisomewa mashtaka mbele ya hakimu mkazi mkuu,Thomas Simba na Hakimu mkazi mkuu, Godfrey Mwambapa.
Wakili wa serikali Mohamed Salum amesema kuwa washtakiwa hao wakiwa eneo la mikocheni kwa nafasi zao wakijua jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa mawasiliano kwa njia ya mtandao kufuatia chapisho lililochapishwa katika tovuti yao na waliamua kushindwa kutoa ushirikiano jeshi la polisi kwa kuwanyima data walizonazo .
Hata upelelezi wa kesi hizo mbili umekamilika na washtakiwa wote hawa watasomewa mashataka yao kuanzia Februari 9 na Februari 20.
Mpaka sasa washtakiwa wote wawili wapo nje kwa dhamana kwa masharti ya bond ya Milioni 10 kwa kila kosa na masharti ya kutosafiri nje ya nchi.
 Mike Mushi akitoka katika chumba cha mahabusu akipandishwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es Salaam
 Maxence Melo na Mike Mushi wakiwa nje ya chumba cha mahakama wakisubiri kuingia ndani
 Maxence Melo akijaribu kumueleza jambo mmiliki mwenza wa Jamii Forum Mike mushi ndani ya chumba cha Mahakama
 Maxence Melo na Mike Mushi wakimsikiliza wakili wao

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad