Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baina ya mahasimu, Simba na Yanga umesogezwa mbele hadi Februari 25, kutoka na Yanga kuwa na mashindano ya kimataifa ambapo itawawia vigumu kucheza siku hiyo.
Mchezo huo uliotakiwa kufanyika Februari 18, mwaka huu umesogezwa mbele kuwapisha Mabingwa hao wa ligi kuu 2015/2016 kumaliza mechi zao dhidi ya Ngaye De Mba ambao utachezwa Februari 10 nchini Comoro na kurudiana Februari 17 katika Uwanja wa Taifa.
Habari kutoka ndani ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba sababu ya kusogezwa mbele kwa mchezo huo ni muingiliano na Ratiba ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika.Februari 10, mwaka huu,
Kwa sababu hiyo, mchezo wa Simba na Yanga usingeweza kufanyika tena Februari 18 na busara za TFF zimeupeleka hadi Februari 25.
No comments:
Post a Comment