Mwakilishi
wa UNOPS Bw Bernard Omondi akifanunua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba katika eneo la Temeke -
Mtoni kwa Azizi Ali ambapo kazi ya kusafisha na kujenga mfumo wa maji taka
inaendelea.
Na Lulu Mussa
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba amefanyia
ziara ya kikazi ya kukagua hatua za ujenzi katika miradi inayofadhiliwa na
Ofisi yake.
Akiwa katika Wilaya ya
Ilala, Waziri Makamba ametembelea ujenzi wa Mfereji wa kupitishia maji taka
katika eneo la Ilala Bungoni na kuongea na wananchi wa eneo hilo.
Waziri Makamba ameugiza
uongozi wa Dezo Civil Constractors Co.
Ltd kuhakikisha ujenzi wa Miundombinu ya maji taka katika
Manispaa za Ilala na Temeke unakamilika kwa muda uliopangwa na kwa ubora wa
hali ya juu kwa kuzingatia makubaliano yaliyopo katika mkataba.
“Nataka mradi huu
uwe wa mfano kwa ubora na viwango vya hali ya juu, ikiwa ni jitihada za
kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi, kwa kuweka mfumo mzuri wa
kukusanya maji taka na kuyaelekeza sehemu stahiki” Makamba alisisitiza.
Aidha, Waziri
Makamba amewataka wakazi wanaozuka eneo hilo kuacha mara moja utupaji wa taka
maji na taka ngumu katika mfereji huo unaojengwa, na kumuagiza Mkurugenzi wa
Manispaa ya Ilala Bw. Palela Msongela kutoa adhabu kali kwa yeyote atakayekiuka
agizo hilo.
“Kwa kupitia kamati
za Mazingira za vitongoji na sheria ndogo ndogo mlizojiwekea hakikisheni kuwa
hifadhi ya mazingira inazingatiwa kwa mstakabali wa vizazi vya sasa na vizazi
vijavyo.”
Pia, Waziri
Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha Wakandarasi
wanaopewa kazi za ukusanyaji wa taka, wanakuwa na vifaa na uwezo wa kutosha kwa
kuhakikisha taka zote zinazolewa kwa wakati ili kuepuka mrundikano wa taka
katika makazi ya watu.
“Natoa wito pia
kwa vijana wa maeneo haya kuunda vikundi vidogo vya kuzoa taka ili kuwa chanzo
cha ajira kwenu.” Makamba alisisitiza.
Waziri Makamba
ameliagiza Baraza la Taifa La Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira - NEMC kutembelea eneo hilo la Ilala Bungoni na
kutoa maelekezo kwa Gereji bubu
zinazokiuka hifadhi na usimamizi wa Mazingira kwa kufanya shughuli zao
pembezoni mwa mfereji unaojengwa.
Ujenzi wa Ukuta
wa (Obama/Ocean Road na Kigamboni) na Miundombinu ya maji taka katika Manispaa
za Ilala na Temeke unatekelezwa chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi na unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa
kuhusu Mazingira (UNEP). Aidha, Kampuni ya Dezo Civil Contractors ndio inafanya
kazi ya ujenzi huu na kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi Julai 2017.
Waziri Makamba
katika ziara yake hii leo ametembelea Ilala Bungoni, Mtoni kwa Azizi Ali, Chuo
cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere na Kutembelea eneo la Ujenzi wa Ukuta Barabara
ya Obama.
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na Diwani
wa Kata ya Buguruni Mhe. Adam Fugame (katikati) wakati wa ziara ya
kikazi ya kukagua ujenzi wa mfereji wa maji taka katika eneo la Ilala Bungoni jijini Dar es salaam
Sehemu ya Mfereji wa Maji
taka unaojengwa eneo la Ilala Bungoni chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais kupitia Mradi wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi
na unafadhiliwa na Shirika la Umoja wa
Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP).
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akiongea na
Wananchi wakazi wa Ilala Bungoni, mara baada ya kukagua ujenzi wa mrefeji wa
maji taka
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu
wa Rais Prof. Faustin Kamuzora ( wa tatu kutoka kulia) akifafanua jambo kwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano na Mazingira Mhe. January
Makamba mara baada ya ziara ya kukagua hatua za ujenzi kwa miradi inayosimamiwa
na Ofisi ya Makamu wa Rais. Kulia ni Bw.
Kanizio Manyika Afisa Mazingira Mkuu na Msimamizi wa Mradi na Bw. Richard
Muyungi Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira.






No comments:
Post a Comment