Msemaji wa Jeshi la polisi,Advera Bulimba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya wananchi kuwa makini pindi wanapofanya biashara kwa njia ya mitandao kwa sababu wananchi wengi wamekuwa wakiibiwa kwa kutokuchukua tahadhari za kutosha,leo jijini Dar es Salaam.
Na Emmanuel Masaka, Globu Jamii.
JESHI la polisi limewataka wafanya biashara kuhakikisha kuwa wanaomba ulinzi kutoka jeshi la polisi au makampuni binafsi ya ulinzi yanayo husika na kusafirisha fedha ilikupunguza matukio ya kuvamiwa na kuibiwa fedha wanapokuwa wakisafirisha.
Akizungumza na waandishi wa habari leo hii Jijini Dar es salaam Msemaji wa Jeshi la polisi Advera Bulimba amesema uchunguzi wa Jeshi la polisi umebaini kuwa uhalifu huo umekuwa ukisababishwa na wafanya biashara husika kutokuwa na usiri pamoja na kutokuomba ulinzi kutoka Jeshi la polisi au makampuni binafsi ya ulinzi yanayoshughulika na kusafirisha fedha.
‘’Jeshi la polisi nchini linatoa wito kwa wafanya biashara kuhakikisha kuwa wanaomba ulinzi kutoka jeshi la polisi aumakampuni binafsi ya ulinzi yanayoshughulika na kusafirisha fedha pia wasafirishaji wa fedha kuwa na usiri katika michakato yote inayohusiana na usafirishaji wa fedha ilikuweza kupunguza matukio ya hayo’’ amesema Advera.
Aidha Msemaji huyo amesisisitiza kuwa wananchi kuwa makini pindi wanapofanya biashara kwa njia ya mitandao kwa sababu wananchi wengi wamekuwa wakiibiwa kwa kutokuchukua tahadhari za kutosha kabla ya kutuma fedha.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Msemaji wa Jeshi la polisi,Advera Bulimba leo jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment