Ukibahatika kukutana na mnyama ambaye anaweza kubadili rangi na ama kuona taswira mbili kwa wakati mmoja hata ziwe pande tofauti jitahidi kujifunza sana maana hiyo ni kama bahati ya mtende kuota jangwani .....huenda vizazi vijavyo vitakuulizwa maswali kwa njia ya PICHA tu kwani wanyama wengi adimu wanatoweka duniani na hakuna ajuaye mustakabali
Kinyonga anaweza kuonekana wa kawaida katika macho ya wengi, lakini kwa wale wanaojali mazingira na urithi wa taifa hii ni kesi kubwa iwapo utamchukulia POA na wanalindwa na sheria za kimataifa za uhifadhi wa viumbe walio hatarini kutokweka (Convention on International Trade in Endangered Species) kama mojawapo ya viumbe WALIO HATARINI KUTOWEKA (mara yako ya mwisho kuona kinyonga ilikua lini?).
Kinyonga ni moja ya wanyama wanaokwenda kuwa adimu sana duniani kuwaona kwa macho (naked eyes)
1. Karibu nusu ya Vinyonga wameshatokweka duniani kwa mujibu wa sensa mbalimbali zinazofanyika kwa njia ya uratibu na sasa yasemekana Madagascar ndiyo nchi pekee yenye karibu aina zote za vinyonga WALIOSALIA (species) ambayo inakadiriwa kuwa 160
2. Vinyonga walio wengi na hasa wanaopatikana Tanzania huweza kubadili rangi kutoka chanikiwiti hadi hudhurungi ama yakuti yasipii na samawi, ingawa ukweli ni kwamba kuna baadhi ya vinyonga wanaweza kubadilika kwa rangi yeyote ile kwa MUDA WA TAKRIBANI SEKUNDE 20 ....hii ni kutokana na kuwa na seli zinazoangazia kwenye ngozi zao zikiwa na uwezo wa kusharabu mwanga/ joto ama kwa kukereka (mood) na si kweli kwamba wanabadili kwa kuakisi mazingira kwa mujibu wa tafiti
3. Jicho la Kinyonga lina uwezo wa kuona TASWIRA mbili kwa wakati mmoja (360 degree) hiki ni kiwango cha juu sana miongoni mwa reptilia na wana uwezo wa kuona wadudu wadogo sana umbali wa mita 5-10
4. Kutokana na aina ya mihanjo yake ya kusakanya mkate wake wa kila siku, Urefu wa Ulimi wa Kinyonga ni MARA MOJA NA NUSU ZAIDI YA UREFU WA MWILI WAKE , ni ngumu sana iwapo wewe ni riziki ya Kinyonga ukakatiza mbele yake hata kwa sekunde moja.
5. Miguu ya Kinyonga imeumbwa kwa namna ambayo inaweza kuparamia mazingira yoyote yale ya miti au miamba yaani iwe ya utelezi au hata miiba.....miguu yake inaweza kukunjika ama kukunjuka KAMA KARATASI kulingana na mazingira (si rahisi sana kuelezea hili zaili ya Muumbaji mwenyewe ) yatosha tu ufahamu ya kwamba Kinyonga anaweza kupita POPOTE PALE.Imeandaliwa na Geofrey Chambua Kutoka Vyanzo mbalimbali
zaidi nenda
No comments:
Post a Comment