HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, January 31, 2017

AZAM FC KUKIPIGA NA MAMELOD SUNDOWN KESHO UWANJA WA TAIFA

 Afisa habari wa Azam Jafar Iddy Maganga.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

KLABU ya Azam imeridhia kucheza na mabingwa wa Afrika Mamelod Sundown baada ya timu za Yanga na Simba kujiondoa na kila mmoja akitoa sababu zake.

Akiyasema hayo, Afisa habari wa Azam Jafar Iddy Maganga amesema kuwa mechi yao na mabingwa hao wa Klabu Bingwa Afrika utafanyika majira ya saa moja usiku kwenye Uwanja wa Taifa ambapo wanategemea kutumia kikosi chao cha kwanza kujipima nao.

Maganga amesema kuwa, mwaka jana walivyoenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini na wakafanikiwa kucheza nao mechi ya kirafiki kwahiyo hawana budi nao kufanya hivyo ingawa wamepata taarifa ya  mchezo huo ikiwa imechelewa.

"tumechelewa kupata taarifa ya mchezo huo, ni jana usiku ila uongozi wa klabu ya Azam umeamua kukubali mechi hiyo ichezwe kesho saa 1 usiku kwani hata sisi mwaka jana tulivyoenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini tuliwaomba mechi na tukacheza nao,"amesema Maganga.

Kwenye mchezo huo wa kwanza wa kirafiki dhidi ya Mamelodi, Azam walifanikiwa kutoka na ushindi wa goli 1-0.


Klabu za Yanga na Simba zimegomea kucheza mechi hiyo ya kirafiki huku Simba wakisema kuwa hawawezi kucheza mechi siku ya Jumatano halafu Jumamosi wakacheze mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji na kwa upande wa Yanga nao wamesema kucheza Ijumaa dhidi ya Mamelod na jumapili wakutane na Stand haiwezekani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad