HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 15, 2016

WATAALAM WA USAFIRI WA ANGA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA ZANZIBAR

 Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza S. Johari akizungumza katika  mkutano wa kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki Unaofanyika  Zanzibar.
 Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Balozi Amani Karume, akifungua  rasmi mkutano wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki uliofanyika Zanzibar leo.
Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar , Balozi Amani Karume, akiwapongeza Wajumbe waliostaafu wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki kwa mchango  wao katika Kamati.
 Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki walipotembelea Kikosi cha Zimamoto katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume(AAKIA) 
 Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Balozi Amani  Karume,(Kulia) akishiriki Mkutano wa 41 wa Kamati ya Uwezeshaji Usafiri wa Anga ya Afrika Mashariki unaofanyika Zanzibar, Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Hamza Johari

Kamati ya kuwezesha na kuboresha usafiri wa anga ya Jumuiya ya Afrika Mashariki imekutana kwa siku tatu mjini Zanzibar  ikiwa ni sehemu ya mikakati ya nchi wanachama kuboresha sekta hii ya uchukuzi katika nchi wanachama.

Mkutano huo wa 41 umefunguliwa  rasmi na Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Ali Abeid Amani Karume, ambaye amesema  miundombinu katika viwanja vingi vya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki vinahitaji kuboreshwa ili kumudu ushindani wa kibiashara katika sekta hii. 

Aidha, amezungumzia umuhimu wa nchi wanachama kupunguza tozo kwa kampuni zinazotoa huduma za usafiri wa anga ili kuvutia uwekezaji zaidi katika sekta.


Waziri huyo  amesisitiza umuhimu wa   watalaam wa usafiri wa anga katika nchi za Afrika Mashariki kupatiwa mafunzo ya kutosha  kuimarisha ujuzi  na uwezo wa utendaji kumudu majukumu yao.

Awali wajumbe zaidi ya 70 wa kamati ya Kuwezesha Usafiri wa Anga katika nchi za Afrika Mashariki walitembelea kiwanja cha Kimataifa cha Abeid Amani Karume (AAKIA) ili kujionea  miundombinu na huduma zinazotolewa katika kiwanja hicho cha ndege.


Wajumbe hao wa kamati ya Afrika Mashariki kutoka nchi za Burundi, Rwanda, Kenya,  Uganda na Mwenyeji Tanzania hukutana mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kujadili  ubora wa utoaji huduma za usafiri  anga kwa abiria na mizigo .

Kamati hiyo hujadili changamoto na kupendekeza suluhu za kuboresha sekta hiyo kwa lengo la kuwezesha sekta hii kutoa mchango katika kukuza uchumi wa nchi wanachama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad