HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 21, 2016

Wanawake ndio waathirika wakubwa katika umiliki wa ardhi ya kilimo nchini.

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Imeelezwa kuwa waathirika wakubwa wa upatikanaji wa ardhi kwa ajili ya kilimo ni wanawake kutokana na mila ,desturi na tabia zilizopo katika jamii yetu.

Swala hilo limeibuka katika mjadala wa kujadili masuala ya kilimo kwa ajili ya wanawake iliyoandaliwa na mtandao wa kijinsia nchini (TGNP) kwa viongozi wa ngazi mbalimbali wa serikali za mitaa.

Akizungumza katika mjadala huo Mwanasheria kutoka wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi,Adelfina Lekule amesema kuwa sheria ya Ardhi namba 4 /1999 inaeleza kuwa kila mtu ana haki ya kumiliki ardhi bila ya kujali jinsia . Hivyo kuweka wazi kuwa kutoka na sheria hiyo kila mtu ana haki ya kumiliki ardhi kma ilivyo katika tafsiri ya sheria hiyo.

"Sera mpya ya ardhi ipo katika mchakato licha ya kuwa atuna sheria ya moja kwa moja ya urithi hivyo ikitokea kuwa kuna mgawanyo mali uangalia aina ya maisha watu wanayoishi au dini na mila na desturi katika eneo husika" amesema Lekule.

Kwa upande wake Mzengezi na Mchambuzi wa warsha hiyo ,Geofrey Chambua ,amewataka wadau hao wa masuala ya kilimo na jinsia kufanya ufuatiliaji wa masuala ya kijinsia hasa katika kuhakikisha mwanamke anapata nafasi ya kumiliki ardhi kwa ajili ya kilimo hili kuweza kuongezantija na kufikia malengo ya kuwa na chakula cha kutosha kufikia 2030.

Aidha katika mjadala huo pia waliweza kuzungumzia ni namna gani masuala ya ndoa hasa juu ya kutambua nani ni mtu sahii anayepaswa kumiliki ardhi pindi mume anapo fariki.

Mwanasheria kutoka Wizara ya Ardhi ,Adelfrida Lekule akizungumza wakati wa mjadala huo ulioandaliwa na TGNP.
Mzengezi na mchambuzi wa masuala ya kijinsia ,Geofrey Chambua akitoa mada wakati wa warsha hiyo iliyoandaliwa na TGNP kwa wadau wa kilimo nchini na wakulima.
Washiriki wakifuatilia mjadala huo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad