HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, December 29, 2016

WAKALA WA VIPIMO KUWEKA STICKER MPYA KWA VIPIMO MBALIMBALI KUANZIA MWAKA 2017

Kaimu Meneja sehemu ya Elimu, Habari na Mawasiliano wa Wakala wa Vipimo, Irene John akizungumza na waandishi wa habari juu ya Uwekaji wa Sticker mpya zitazoanza kutumika mwakani. 

Mkurugenzi wa Ufundi Bi. Stella Kahwa akionyesha kwa Waandishi wa Habari Sticker zitakazoanza kutumika hapo mwakani

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAKALA wa Vipimo (WMA) inatarajia kuweka Sticker katika vipimo mbalimbali ili kuweza kumlinda mlaji kwa huduma inayoendana na thamani fedha yake.

Akizungumza na waandishi wa habari  leo jijini Dar es Salaam, Kaimu Meneja Sehemu ya Elimu , Habari na Mawasiliano, Irene John amesema uwekaji Sticker utaanza rasmi mwaka ujao kwa kubandika sticker hiyo kwa kila kipimo ambacho kinatambulika na Wakala Vipimo. Amesema sticker hizo zitawekwa katika pampu zinazotumika katika vituo vya vya mafuta ambavyo vitakuwa vimehakikiwa ili mteja ajue uhalali wa kipimo hicho na mafuta.

Irene amesema mlaji akiona sticker katika kituo cha mafuta afahamu kituo hicho kimehakikiwa na wakala wa vipimo. Amesema katika uwekaji wa sticker huo ni pamoja bohari za Mafuta kwa kuweka sticker maalumu katika kipimo cha mafuta 'flow Meters' zitakazotumika kujaza mafuta katika magari ya kubebea mafuta itafanya wabebaji wa mafuta kwa magari wataweza kutambua kipimo hicho kilivyohakikiwa.

Hata hivyo amesema katika jitihada hizo hufanya uhakiki wa mizani yote kuhakikisha inapima kwa usahihi ikiwa ni pamoja na kuweka sticker maalumu. Irene amesema mizani yote inayotumiwa na wafanyabiashara itahakikiwa ili kujua usahihi wake na uhakiki wake utakuwa ni kugonga mhuri na kuweka sticker.

Amesema mazao yote watahakiki mizani ya wafanyabiashara na mizani ambayo itakuwa haina sticker wakulima wasitumie na wanatakiwa kutoa taarifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad