HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, December 21, 2016

VIJANA WA KITANZANIA WAHIMIZWA KUCHANGAMKIA FURSA

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Vijana wa kitanzania wahimizwa kutambua fursa za kiuchumi na kupambana na changamoto mbalimbali za kiuchumi zinazowazunguka na kujihusihsa katika shughuli  ili kuweza kujiletea maendeleo na kupunguza umaskini.

Akizungumza wakati wa semina elekezi ya vijana iliyoendeshwa na Taasisi ya MIBOSCO wakati wa ufunguzi wa jukwaa la uchumi ka kuwawezesha vijana kiuchumi na kuwakutanisha takribani vijana 200, Afisa Vijana Mkoa wa Dar es salaam Nasalida Njashi amesema kuwa vijana wanatakiwa waache uoga wanatakiwa kujitokeza mbele ili kuweza kupambana na changamoto mbalimbalikwa ajili ya kuleta maendeleo.

Njashi amesema hayo mbele ya Mkurugenzi Mkuu wa MIBOSCO Moses Meena na kuwataka viongozi hao kutokaa nyuma na kusubiri misaada bali wanatakiwa waunde vikundi vya vijana wachache ili kuweza kupata mikopo ya riva nafuu kutoka kwenye mfuko wa serikali wa fungu la asilimia kumi kwa ajili ya vijana na wanawake ambapo itawasaidia kwenye kuanzisha miradi mbalimbali.

Mkurugenzi Mkuu wa MIBOSCO Moses Meena amesema kuwa jukwaa lao limedhamiria kuleta mwamko na hamasa chanya kwa vijana na katika harakati za kujikomboa kiuchumi na mafunzo hayani mwendelezo wa shughuli zinazofanywa na Taasisi hiyo ikiwa ni harakati za kupambana na umaskini.

Katika jukwaa hilo kulikuwa na Afisa kutoka Baraza la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi George Maura na kuwataka vijana kuacha kusubiri kuanzishiwa miradi au masuala mbalimbali ya kiuchumi na kuwataka kuunda umoja wao kwa ajili ya kupata mikopo kutoka serikali, pamoja na kuwapatia sifa uongozi wa MIBOSCO kwa juhudi kubwa za kuwapatia ellimu ya ujasiriamali vijana wa Kunduchi Mtongani.

Jukwa hilo lilihudhriwa pia na mtangazaji wa Clouds Maoud Kipanya, Wawakilishi kutoka NSSF na benki ya ACB kama wadau wa maendeleo.
Afisa Vijana Mkoa wa Dar es salaam Nasalida Njashi akizungumza na vijana wakati wa jukwaa la uchumi la kuwawezesha vijana kiuchumi liloandaliwa na Taasisi ya MIBOSCO.
 Afisa Vijana Mkoa wa Dar es salaam Nasalida Njashi (katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa MIBOSCO Moses Meena (kushoto), Afisa wa Baraza la Taifa la uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi George Maura, Meneja wa NSSF Tawi la Mbezi Beach Stella Kabyemela na Mwakilishi kutoka benki ya ACB.

 Viongozi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana waliojitokeza kwenye Jukwaa la uchumi la kuwawezesha vijana kiuchumi.
Afisa Vijana Mkoa wa Dar es salaam Nasalida Njashi akiangalia baadhi ya bidhaa zilizotengezenezwa na vijana wajasiriamali walio chini ya MIBOSCO.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad