Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
MBUNGE wa Mkuranga, Abdallah Ulega amefanya ziara katika vijiji vya Kisayani na Msorwa ili kujua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na kuweza kuzishughulikia kupitia Halmashauri pamoja Ofisi yake.
Akizungumza na wananchi waVijiji hivyo amesema wakati wa sasa ni kufanya maendeleo ya kweli bila kuangalia itikadi za vyama.
Ulega amesema Mkuranga inahitaji maendeleo kutokana na kukaa muda mrefu bila kuwa na mabadiliko ya wananchi katika huduma za jamii kutokana na viongozi
Amesema kazi yake ni kuhamasisha wananchi katika masuala ya maendeleo pamoja na kupokea na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali za wananchi wa vijiji hivyo
Katika ziara hiyo, amepokea changamoto mbalimbali ikiwemo ubovu wa miundominu ya barabara, Afya, Elimu, Umeme pamoja na Maji ambapo amewahakikishia wananchi hao kuzishughulikia changamoto hizo zinazo wakabili ili kuchochea maendeleo ya vijiji hivyo.
Ulega amesema ameweza kufanya ziara katika vijiji 90 kati ya vijiji 125 katika Jimbo la Mkuranga ambapo kati ya vijiji hivyo asilimia 50 changamoto zimetatuliwa.
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisayani alipokwenda kuwatembelea pamoja na kuangalia maendeleo ya kijiji hicho leo .(picha na Emmanuel Massaka ,Globu ya Jamii)
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kisayani, Siasa Kibende akizungumza katika wananchi wa kijiji hicho walipotembelewa na Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega alipokwenda kuwatembelea pamoja na kuangalia maendeleo leo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga, Juma Abeid akizungumza na wananchi wa Vijiji vya Kisiyani na Msorwa katika ziara ya Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega leo.
Diwani wa Kata ya Mbezi, Mkuranga, Rashid Selungwi akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Msorwa katika ziara ya Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega leo.
Mkazi wa Kijiji cha Kisiyani Kata ya Mbezi, Joel Kianga akichangia mada katika ziara ya Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega leo .
Mkazi wa Kijiji cha Msorwa Kata ya Mbezi, Kautila Kautila akichangia mada katika ziara ya Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega leo .
Sehemu ya wananchi wa kijiji cha Kisiyani wakimsikiliza Mbunge wa Mkuranga , Abdallah Ulega
Mbunge wa Mkuranga, Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mkuranga,Juma Abeid, pamoja na Diwani wa Kata ya Mbezi, Rashid Selungwi wakagua ghala la kuifadhia korosho katika kijiji cha Msorwa kata ya Mbezi. (Picha na Emmanuel Massaka ,Globu ya Jamii)

No comments:
Post a Comment