Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BENDI ya muziki wa dansi nchini African Star "Wana Twanga Pepeta" , watasindikiza utambulisho wa bendi mpya ya muziki wa taarabu Yah TMK Modern, utaofanyika Desemba 17 mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Dar Live, uliopo Mbagala Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa bendi hiyo Said Fella, alisema kuwa Twanga Pepeta watakuwepo kusindikiza utambulisho wa bendi hiyo ambayo ni mpya kabisa katika muziki wa taarabu hapa nchini.
Alisema kuwa licha ya kuwepo Twanga Peoeta bado wanafanya mazunguko wa baadhi ya wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya ambao nao watasindikiza usiku huo maalum wa Yah TMK Modern Taarab.
Alisema onesho hilo la utambulisho limeandaliwa na kampuni ya Mkubwa na Wanawe ikishirikiana na Usher family entertainment, ikiwa na wasindikizaji mbalimbali.
"Tunafanya utambulisho rasmi wa bendi yetu ambao tutaufanya Desemba 17 mwaka huu, maandalizi yanaendelea tumeshapata Twanga Pepeta ambao watasindikiza,Yah TMK Modern Taarab"alisema Fella.
Ujio wa bendi hiyo unafuatia baada ya kambi ya nguvu ya takriban mwezi mmoja na nusu, hatua iliyozalisha nyimbo mbili kali “Sina Pupa” wa Mwanahawa Ali na “Kibaya Kina Mwenyewe” wa Aisha Vuvuzela. Yeah TMK inaundwa na wasanii wengi waliojiengua kutoka Jahazi kama vile Mohamed Mauji na Chidy Boy.
Wengine ni Babu Ali, Fatma Mcharuko na Aisha Vuvuzela, Omar Teggo na Mauwa Teggo.
No comments:
Post a Comment