Na Amina Kibwana, Blogu ya Jamii
Serikali ya Tanzania imepokea pokea msaada wa hundi ya dola 50,000 (Dola elfu hamsini) kutoka katika ubalozi wa jamuhuri ya Korea kwa ajili ya kukabiliana na athari zilizotokana na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera, ili kuweza kurekebisha Miundo mbinu,makazi ya watu pamoja na shule.
Serikali ya Tanzania imepokea pokea msaada wa hundi ya dola 50,000 (Dola elfu hamsini) kutoka katika ubalozi wa jamuhuri ya Korea kwa ajili ya kukabiliana na athari zilizotokana na tetemeko la ardhi Mkoani Kagera, ili kuweza kurekebisha Miundo mbinu,makazi ya watu pamoja na shule.
Akizungumza na waandishi wa habari Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki kikanda na Kitaifa Dk. Augustine Mahinga amesema serikari ya korea ni mdau mkubwa hasa ktk misaada ya kimaendeleo, kiuchumi , ustawi wa jamii na katika misaada ya kibinadamu ikiwa ni pamoja kusimamia ujenzi wa hospitali ya logazila na chanika.
“Tumekuwa tukipokea misaada mbalimbali kutoka kwa marafiki lakini huu ni mchanngo wa hivi karibuni kutoka kwa wenzetu wa korea ambapo leo nimepokea hundi hii kwa niamba ya waziri mkuu na serikali ya Tanzania kwa ujumla.”
Hata hivyo Dk Mahinga aliongeza kuwa hundi hiyo ni zawadi kubwa kwa wanachi wetu hasa wa kagera pamoja na kutoa shukrani zake kwa balozi wa korea na kuahidi kuwa kuendelea kufanya kazi kwa pamoja.
Kwa upande wake balozi wa jamuhuri ya korea song Young amesema kuwa kutokana na ushirikiano wao wa muda mrefu Korea imeamua kutoa msaada huo, Korea imeamua kwamba katika kuendeleza ushirikiano wa maendeleo na nchi za afrika Tanzania itapewa kipaumbele na kuwa ni chi ya kwanza kwa afrika ili kudumisha ushirikiano kati ya Jamuhuri ya Korea na tanzania.
Huu ni mwaka wa 25 tangu jamuhuri ya korea kuanzisha ubalozi wao nchini Tanzania,ambapo ili kudumisha ushirikiano huo, Serikali ya Tanzania kupitia Rais wake Dk John Pombe Magufuli nayo inatarajia kuanzisha ubalozi wake huko soo mji mkuu wa korea kusini mapema mwaka 2017.

No comments:
Post a Comment