HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 16, 2016

SEREKALI IMEAMUA KUPELEKA WANASHERIA VIJANA WATAKAO JITOLEA KATIKA WILAYA ZOTE ZA DAR ES SALAAM

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wanasheria vijana watakao jitolea katika wilaya zote za Dar es salaam ili kuwasaidia wananchi katika maswala ya kisheria leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
Mkuu wa Wilaya Temeke Mh.Felix Lyaniva akimshukuru Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kwa ubunifu wake wakupeleka wanasheria katika kila wilaya zote za Dar es salaam ili kuwasaidia wananchi katika maswala ya kisheria leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda akiwa katika picha ya pamoja na wakuu wilaya na wanasheria leo jijini Dar es Salaam.

Na Antony John Globu ya Jamii
Kutokuielewa sheria kumeonekana kunaleta changamoto kubwa kwa jamii hali inayosababisha wananchi kukosa haki zao na kusababisha mlundikano wa kesi mahakamani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amesema kutokana na changamoto hiyo serekali imeamua kupeleka wanasheria vijana watakao jitolea katika wilaya zote za Dar es salaam ili kuwasaidia wananchi katika maswala ya kisheria.

Makonda amesema kati ya changamoto zinazowakabili wananchi wengi ni pamoja na malalamiko ya rushwa katika vyombo vinavyotoa haki, ucheleweshwaji wa kesi mahakamani, migogoro ya ardhi, migogoro ya ndoa, miradhi na waajiri kuwaachisha kazi waajiriwa bila kufuata taratibu.

Aidha amewaambia wanasheria hao kuwa wanatakiwa kutoa msaada wa kisheria kwa watu na makundi ya watu wasio na uwezo katika mashauri ya madai ya jinai, kushughulikia malalamiko mbalimbali juu ya utoaji haki kutoka kwa wananchi na kuwaelekeza pamoja na kuwaelimisha wapi waende kupata suluhu ya haki zao.

Hata hivyo mkuu wa wilaya amesema swala la uandikaji wa miradhi ni changamoto kwa jamii hivyo ni vyema wananchi wakapata msaada huo wa kisheria ili kupunguza changamoto mbalimbali za mashauri yanayohusiana na maswala ya miradhi.

"kati ya mambo munayotakiwa kufanya yaani wajibu wenu pia ni pamoja na kuandika nyaraka tofauti za kisheria kama kuandika wosia, mikataba pamoja na kutoa msaada kwa njia ya simu’’ amesema Makonda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad